Katibu
Mkuu Prof.Makubi akiwa na Viongozi kutoka KOFIH mara baada ya kutia
saini maeneo ya mashirikiano baina ya nchi hizo mbili
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof.Abel Makubi akiwa na Naibu Mwakilishi
Mkazi kutoka Korea Foundation for International Healthcare(KOFIH),Bi.Kim
Jungyoon Kwenye ofisi za Wizara zilizopo mji wa Serikali Mtumba.
Katibu
Mkuu Prof.Makubi akiwa na Mwakilishi Mkazi wa Taasisi ya KOFIH kutoka
Korea ya Kusini Bw.Ha,Seung Rae(kushoto) na Naibu Mwakilishi Mkazi
Bi.Kim Jungyoon(katikati) wakati wa kutia saini makubaliano ya
mashirikiano Kati ya Wizara ya Afya na Taasisi hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto-Idara Kuu Afya Prof.Abel Makubi, leo amekutana na kufanya mazungumzo na Bw. Ha Seung Rae, Mwakilishi Mkazi wa Taasisi ya Serikali ya Korea Kusini (Korea Foundation for International Healthcare-KOFIH) Kwenye ofisi za wizara zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Katika mazungumzo yao pia wametia saini makubaliano mapya baina ya nchi hizo mbili Katika maeneo mapya ya ushirikiano ikiwemo mafunzo na kuijengea uwezo maabara ya Taifa ya Jamii.
Hata hivyo Prof.Makubi ametumia muda huo kwa kuwashukuru KOFIH kwa ushirikiano wao na Serikali Katika kipindi Cha kukabiliana na janga la Corona mwaka jana.
KOFIH ni Taasisi iliyopo chini ya Wizara ya Afya nchini Korea Kusini ambapo inashirikiana na Wizara ya Afya Tanzania Katika maeneo ya kuimarisha mifumo ya Sekta ya afya, Mradi wa kutoa ushauri, mafunzo kwa wataalam pamoja na mafunzo kwa upande wa injinia wa vifaa tiba.
No comments:
Post a Comment