Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Songea Mjini Dkt. Damas Ndumbaro ( kushoto) akimkabidhi funguo na kadi ya gari ya kubebea wagonjwa kwa Dkt. Amos Mganga litakalotumika kwa ajili ya kubebea Wagojwa kwenye kituo cha Afya cha Mji Mwema kilichopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea ikiwa ni miongoni mwa magari 10 ya kubebea wagonjwa yaliyokabidhiwa kwa Wabunge ikiwa ni muendelezo wa jitihada za dhati za Serikali za kuhakikisha Wananchi wanapata huduma bora za afya karibu na makazi yao. Magari hayo 10 ni kati ya magari 50 ya kubebea wagonjwa yenye thamani ya sh.bilioni sita yaliyonunuliwa na Wizara ya Afya,Maendelei ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Global Fund. Makabidhiano hayo yamefanyika leo tarehe 8 Juni, 2021 Jijini Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Songea Mjini Dkt. Damas
Ndumbaro ( katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwakilishi wa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Deogratius Shayo ( wa pili kulia) pamoja na Maofisa wengine
kutoka Wizara ya Afya, ikiwa ni miongoni mwa magari 10 ya kubebea
wagonjwa yaliyokabidhiwa kwa Wabunge ikiwa ni muendelezo wa jitihada za
dhati za Serikali za kuhakikisha Wananchi wanapata huduma bora za afya
karibu na makazi yao. Magari hayo 10 ni kati ya magari 50 ya kubebea
wagonjwa yenye thamani ya sh.bilioni sita yaliyonunuliwa na Wizara ya
Afya,Maendelei ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Global Fund.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo tarehe 8 Juni, 2021 Jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment