ANGALIA LIVE NEWS

Monday, June 21, 2021

UWT wilaya ya Njombe yafanikiwa kuongeza kiwango cha makusanyo kwenye vyanzo vyake vya mapato

 


Na Amiri Kilagalila, Njombe

Jumuiya ya umoja wa wanawake UWT ccm wilaya ya Njombe imesema imefanikiwa kuongeza kiwango cha makusanyo  katika vyanzo vyake toka milioni 94 kwa kipindi kilichopita hadi zaidi ya shilingi milioni 100 kutokana na jitihada kubwa zinazofanywa na viongozi pamoja na wanachama wake.

Katika kikao cha baraza la  jumuiya hiyo katibu wa UWT wilaya ya Njombe Sauda Mohamed katika taarifa yake amesema fedha hizo zinapatikana kutoka kwenye vyanzo vyake mbalimbali vya mapato ikiwemo ukodishwaji wa vibanda vya biashara pamoja na ubinifu wa vyanzo vipya vya mapato.

“Jumla ya mapato yetu kwa mwaka mzima ni milioni mia moja laki tano na arobaini na awali jumuiya ilikuwa inakusanya mapato milioni tisini na nne kwa sasa imeongezeka”alisema  Sauda

Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Njombe Beatrice Malekela amesema sera yao ya kuwawezesha wanawake ili waondokane na utegemezi imeanza kufanyiwa katika katika kata mbalimbali wilayani humo.

“Sera ya CCM ni pamoja na kuhakikisha wanawake wanajiunga na vikundi vya wajasiriamali kwa hiyo tulipopota kweye kata ndani ya majimbo yote tumeona namna wanawake wanavyoendelea kuunga mkono juhudi za kujiwezesha kiuchumi”alisemaBeatrece Malekela

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Njombe Pindi Chana katika kikao hicho cha baraza  amesema ni muhimu kuendelea kushikamana katika shughuli mbalimbali ikiwemo kuungana katika kuviwezesha vikundi mbalimbali hatua ambayo itawasaidia kusonga mbele.

Kwa upande wake mwenyekiti wa UWT mkoa wa Njombe Skolastika Kevela licha ya kupongeza jitihada kubwa zinazofanywa na jumuiya hiyo wilaya lakini ameonesha kusikitishwa na uhai wa wanachama  kwani wengi wao wanashindwa kulipa ada jambo ambalo linakwamisha jitihada za chama na jumuiya yenyewe.

No comments: