ANGALIA LIVE NEWS

Monday, June 21, 2021

Wakuu Wa Wilaya Mkoani Tanga Waahidi Kushughulikia Kero Za Wananchi Kwa Kasi

Mkuu wa mkoa wa Tanga amewaapisha wakuu wa Wilaya wapya wapatao wanne kati ya nane waliochaguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Wakuu hao walioamishishwa vituo vya kazi na kwenda katika Wilaya za Tanga ni pamoja na Hashim Mgandilwa  mkuu wa Wilaya Tanga ,Ghaibu Bullet lingo, mkuu wa Wilaya ya Pangani, Mh Abel Yeji Busalama, Mkuu wa Wilaya kilindi  Mh Siriel Shaidi Nchembe, Mkuu wa Wilaya Handeni .

Wapya ni Basila kalubha Mwanukuzi Mkuu wa Wilaya  korogwe, kalisti Lazaro Bukhay Mkuu wa Wilaya Lushoto, na Halima Abdallah Bulembo kuwa mkuu wa Wilaya ya Muheza mkoani Tanga .

Akizungumza mara baada yakuwaapisha wakuu hao wa wilaya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam kighoma Ali Malima amewasisitiza wakuu wa Wilaya wote kufanya kazi kwa kufuata maadili na kujiepusha rushwa na kuvaa  mavazi ya heshima kujiepusha na unywaji wapombe kupitiliza,

Aidha kwa mujibu wa Malima aliwataka kutokutembea na watoto wa shule na wenye umri mdogo pia kujifanya miungu watu na kuchukua Mali za wananchi kwa kutumia nguvu kinyume na maadili ya uongozi.

Amesisitiza pia wakuu wa Wilaya kujikita katika kutatua migogoro ya wananchi kuafuata katika makazi yao na sio kusubiri viongozi wa juu kufika katika Wilaya zao pia kusimamia kilimo kwani mkoa wa Tanga unategemea kilimo kwa kiasi kikubwa.

Aliwataka Kuakikisha halmashauri zote zinakusanya mapato ya kutosha na kusaidia jamii ikiwemo vijana na kina mama kupata asilimia kumi zilizowekwa kisheria na kusaidia katika kujikimu na maisha na mikopo ya riba nafuu.

 Kwa upande wao wakuu wa Wilaya walioapishwa na kula kiapo wamesema kwamba wapo tayari kuwatumikia wananchi na kufuata maadili ya utumishi wa umma na sio vinginevyo na kamwe hawatamuangusha Mh.Rais.

 Akiongea Mara baada ya Kuapishwa mapema Asubuhi Kalisti Lazaro Mkuu wa Wilaya ya Lushoto amesema Wilaya yake itahakikisha inakuwa kwa kasi hususani katika sekta ya elimu afya na miundo mbinu ya barabara pamoja na Wilaya kuwa na maendeleo ya haraka kwa kutumia ilani ya chama cha mapinduzi ambayo walielezea kwa wananchi kutatua matatizo yote yanaowakabili

No comments: