Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
Mradi wa mabasi ya mwendokasi umeongeza ruti za safari za mabasi hayo na sasa umeanza kutoa huduma zake hadi stendi ya Kibaha na mengine yakifika hospital ya MUHAS Mloganzila.
Kufuatia kuongezwa kwa ruti hizo wakazi wa Kibaha na maeneo jirani wamepongeza Serikali kwa kukomboa wanyonge wakiwemo wanafunzi kwa kusogeza huduma ya uhakika ya usafiri.
Katika vituo vya Mailmoja ,Kibamba , Mloganzila wameonekana watoa huduma ambapo wananchi wamejitokeza kwa wingi.
Mkazi wa Mailmoja Salehe Issa alieleza ,Ni rahisi kwao kutoka Kibaha wakifika hapo wanaunganisha usafiri wa mabasi hayo katika njia kuu za Kimara na Kwingine hali ambayo imesaidia kwa kiasi kikubwa katika utoaji nauli na muda.
“Tunaushukuru uongozi wa mabasi ya mwendokasi (UDART) kwa kutuleteaa usafiri kutokeaKimara hadi Maili Moja Kibaha”Tulikuwa tukipata usumbufu kutokea Mbezi kuja hapa kwa kuzuiliwa tusipande mabasi madogo hadi abiria wa mbali wapande kwanza”
Nae Ramadhan Kazembe alieleza ,Mbezi tulikuwa haturuhusiwi kupanda hadi abiria kuanzia Picha ya Ndege hadi Mlandizi wakae kwenye viti na wakishakaa abiria wa Maili Moja ndiyo wapande.
“Hizi coaster za kutuambia mpaka wajaze halafu sisi wa Maili Moja tusimame walikuwa kweli hawatutendei haki bora tutapumzika na manyanyaso ,” alisema Ramadhan Kazembe.
Mkazi mwingine, Tumaini Thonya alifafanua, ana amani kwani jamaa wananyanyasa sana kauli mbovu ,ubabe hawajui mlemavu, mzee, mjamzito wala wenye vichanga .
Thonya alibainisha, daladala hasa kutoka kule kuja huku wale wanaosema hawapakii Maili Moja Kibaha kimara 650 na Kariakoo 1,300 sasa wamepata kiboko yao.
Kwa upande wake Mohamed Lipwai alisema kuwa usafiri huo ni wa uhakika na ni furaha maana waliteseka kwenye daladala ilikuwa ikifika jioni hawataki kupakia abiria wa Maili Moja wakidai nauli yao ya shilingi 500 ni ndogo.
Amina Ally alisema ,hata wangesema 3,000 kuliko panda shuka panda shuka mbona walikuwa wakipanda panda sana noah kutoka Kariakoo hadi Mbezi 5,000 na Kimara bajaji kwa 2,000 hivyo kwao ni furaha na wanawapongeza kwa hatua hiyo.
Mradi huo ulioanza kazi rasmi kwa majaribio mwaka 2016 , umesaidia kupunguza adha ya usafiri kwa wakazi hususani waishio Kimara na Mbezi licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali ikiwemo uchache wa mabasi.
Ruti zilizokuwepo ni pamoja na Mbezi-Kivukoni, Mbezi-Gerezani, Kimara-Kivukoni, Kimara-Gerezani, Kimara-Morocco.
Nyingine ni Morocco-Gerezani, Morocco-Kivukoni ,Muhimbili-Gerezani na Kawe.
Wakati unaanza ulikuwa na mabasi 140 na unaendeshwa na kampuni binafsi ya Udart huku DART ikibaki kama msimamizi wa miundombinu.
No comments:
Post a Comment