Baadhi ya washiriki wapatao 15 wa shindano la kuwania taji la miss Pwani kwa mwaka wa 2021 wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa katika maandalizi ya kinyng’anyoro hicho ambacho kinatarajiwa kufanyika siku ya kesho ijumaa Wilayani Kibaha
Mmoja wa washiriki wa shindano la kumsaka mlimbwende wa miss Pwani 2021 Sara akiwa katika pozi baada ya kumaliza kufanya mazoezi
NA VICTOR MASANGU, PWANI
KINYANG’ANYIRO cha shindano ambalo lilikuwa linasubiliwa kwa hamu na shauku kubwa la kumsaka mlimbwende atakayewania taji la miss Pwani linatarajiwa kufanyika siku ya kesho ijumaa katika ukumbi wa Destiny hall uliopo eneo la kwa mathias Wilayani Kibaha.
Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano maalumu ambao ulioandaliwa kwa ajili ya kuwatambulisha warembo hao mkurugenzi mtendaji wa Twiga Enternment Mariam Sheiban aka (Twiga) ambaye pia ndiye mwandaaji wa shindano hilo amebainisha kuwa maandalizi yote mpaka sasa yameshakamilika.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa katika shindano hilo jumla ya walimbwende wapatao 15 kutoka wilaya mbali mbali za Mkoa wa Pwani watashiriki katika siku hiyo ambapo watapanda jukwaani katika kuonyesha mavazi ya ubunifu, vazi la ufukweni pamoja na vazi la usiku sambamba na kuonyesha vipaji walivyonavyo.
“Maandalizi ya shindano letu la kumsaka miss Pwani kwa mwaka huu wa 2021 yanakwenda vizuri na mipango yote tumeshaifanya na warembo wote wamekaa kambini wakijifua tangu agosti 28 mwaka huu wakiwa wanajifua katika eneo la Art Hotel hivyo imani yangu siku hiyo mashabiki watapata burudani ya aina yake,”alisema Twiga.
Aidha aliongeza kuwa katika shindano hilo litaweza kupambwa na burudani mbalimbali za wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya pamoja na burudani nyingine kutoka kwa bendi ya muziki wa dansi kutoka kwa Ruvu stars ambao watashusha burudani ya aina yake ambayo haijawahi kutokea
Akifafanua kuhusiana na suala la kiingilio alibainisha tiketi za kawaida watakata kiingilio cha shilingi 10,000 /=(SILVER), ambapo katika viti vya kawaida vitalipiwa kiasi cha shilingi elfu 35,000 /= (PLUTINUM), huku viti maalumu (VIP) tiketi zake zitauzwa shilingi elfu 50,000/= (GOLD) na kwamba zimeshaanza kuuzwa katika baadhi ya vituo.
Kwa upande wa wadhamini Twiga Enternment,Mtanga Poly Machiner,Anne Stationar , Kiteshe Lodge&Pub,Marrgap-makeup,Gnail,Hair Reluxer, Destiny Hall, Meeting Point, Art Hotel, Kiduli Security,Black Eye Sucurity, Recho Collection, pamoja na Smart Studio.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo aliwaomba mashabiki na wadau mbali mbali wa fani hiyo ya ulimbwende kujitokeza kwa wingi katika shindano hilo na kwani pia kutakuwa na burudani nyingine ambazo zitafanyika za wasanii kutoka Mkoa wa Pwani.
No comments:
Post a Comment