Advertisements

Wednesday, September 8, 2021

WAKANDA ILIVYOTIKISA JIJI LA NEW YORK

Katika kuendeleza kiutangaza Tanzania na Afrika kwa ujumla ikiwemo mila na tamaduni za Mwafrika, familia ya Luangisa waishio Mt. Vernon, New York Jumamosi ya Sept 4, 2021 walifanya tamsha la kukata na shoka linalobeba jina la Wakanda Celebration na kuhudhuriwa na Balozi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa, Mhe.Gaston Kennedy pamoja na Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa, Brigedia Jenerali George Itang'are. Wengine waliohudhuria tamasha hilo ni Meya na mwakilishi wa Bunge la Marekani. Katika tamasha hilo Dj Dennis Shengena alisherehesha shughuli hiyo akishirikiana na bendi mbalimbali zenye asili na tamaduni za kiAfrika.
Mlimbwende akipita kuonyesha kivazi cha kiafrika mbele ya umati wa watu waliofika kuhudhuria tamasha hilo lililofana kupita maelezo,
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi.
Picha zaidi baadae

No comments: