ANGALIA LIVE NEWS

Friday, October 1, 2021

JKCI KWA KUSHIRIKIANA NA HOSPITALI YA WILAYA YA KIGAMBONI WAADHIMISHA SIKU YA MOYO DUNIANI KWA KUPIMA MAGONJWA YA MOYO BILA MALIPO KWA WANANCHI

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Fatma Nyangasa akizingumza na wananchi waliofika katika viwanja vya Hospitali ya wilaya ya Kigamboni iliyopo eneo la Gezaulole jijini Dar es Salaam kwa ajili ya upimaji wa magonjwa ya Moyo bila malipo uliofanywa na wataalamu kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Kigamboni ni maadhimisho ya siku ya moyo Duniani.
Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Kigamboni wakimsikiliza mkuu wa wilaya hiyo Fatma Nyangasa wakati akizungumza nao kuhusu umuhimu wa kupima afya wakati wa upimaji wa magonjwa ya moyo bila malipo uliofanyika katika viwanja vya Hospitali ya wilaya ya Kigamboni ikiwa ni maadhimisho ya siku ya moyo Duniani.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Fatma Nyangasa akimsikiliza Alex Kyando kutoka kampuni ya uagizaji na usambazaji wa dawa za binadamu na vifaa tiba ya Ajanta Pharma Limited alipokuwa akimweleza kuhusu aina ya dawa za moyo wanazozitoa kwa watu waliokutwa na matatizo ya moyo wakati wa upimaji wa magonjwa ya moyo bila malipo uliofanywa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Kigamboni ikiwa ni maadhimisho ya siku ya moyo Duniani.
Mtafiti kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Makrina Komba akimweleza Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Fatma Nyangasa jinsi wanavyowapima na kupata uwiano wa urefu na uzito wananchi waliofika katika Hospitali ya wilaya hiyo wakati wa upimaji wa magonjwa ya Moyo bila malipo uliofanywa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Kigamboni ikiwa ni maadhimisho ya siku ya moyo Duniani.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Fatma Nyangasa akiangalia picha inayoonesha mlo kamili wakati Afisa lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Husna Faraji alipokuwa akimwelezea kuhusu lishe bora wakati wa upimaji wa magonjwa ya Moyo uliofanywa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Kigamboni ikiwa ni maadhimisho ya siku ya moyo Duniani.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mourice Obwanga akimpima shinikizo la damu (BP) mwananchi aliyefika katika viwanja vya Hospitali ya wilaya ya Kigamboni kwa ajili upimaji wa magonjwa ya Moyo uliofanywa na wataalamu wa Taasisi hiyo kwa kushirikiana na wenzao wa Kigamboni ikiwa ni maadhimisho ya siku ya moyo Duniani.
Mkazi wa Kigamboni akisoma Jarida la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) linalotoa uelewa wa magonjwa ya moyo wakati wa upimaji wa magonjwa ya moyo bila malipo uliofanywa kwa wakazi wa wilaya hiyo na wataalamu JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Kigamboni ikiwa ni maadhimisho ya siku ya moyo Duniani
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Fatma Nyangasa akiangaliza dawa ya moyo iliyokuwa inatolewa bila malipo na kampuni ya uagizaji na usambazaji wa dawa za binadamu na vifaa tiba ya Samiro Pharmaceutical Limited kwa watu waliokutwa na matatizo ya moyo wakati wa upimaji wa magonjwa ya moyo uliofanywa kwa wakazi wa wilaya hiyo. Kulia ni mwakilishi wa kampuni hiyo Faraji Namonde.
Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Tulizo Shemu akimwonesha aina ya dawa za moyo alizomwandikia mkazi wa Kigamboni wakati wa upimaji wa magonjwa ya Moyo bila malipo uliofanywa na wataalamu wa Taasisi hiyo kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya wilaya ya Kigamboni ikiwa ni maadhimisho ya siku ya moyo Duniani.
Maafisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni wakitoa huduma za upimaji wa magonjwa ya Moyo bila malipo kwa wananchi wa wilaya hiyo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya moyo Duniani.
Daktari wa Hospitali ya wilaya ya Kigamboni James Mbapila akiwaeleza madhara ya magonjwa ya moyo wananchi waliofika katika viwanja vya Hospitali hiyo jana kwa ajili ya upimaji wa magonjwa ya moyo bila malipo uliofanywa na wataalamu wa Hospitali hiyo kwa kushirikiana na webzao wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) .

Picha na JKCI

No comments: