ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, October 28, 2021

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AZINDUA KAMPENI YA MADAWATI 1000 YA BENKI YA EXIM

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (Kushoto) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Tanzania Bw Jaffari Matundu wakiwa wameketi katika moja ya madawati yaliyotolewa na benki ya Exim Tanzania kwa ajili ya Mkoa wa Lindi yakiwa ni sehemu kampeni ya ugawaji madawati 1000 yaliyofadhiliwa na benki hiyo kwa ajili ya shule za msingi katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dodoma, Mtwara, Lindi, Mbeya, Mwanza na Tanga wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika Mkoani Lindi jana. Wanaoshuhudia ni pamona na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bi Zainabu Telack (Kulia) na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim Bw Stanley Kafu (Kushoto)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (Katikati) akikata utepe kuashiriki uzinduzi wa kampeni ya ugawaji madawati 1000 ya Benki ya Exim Tanzania kwa ajili ya shule za msingi katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dodoma, Mtwara, Lindi, Mbeya, Mwanza na Tanga wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika Mkoani Lindi jana. Wanaoshuhudia ni pamona na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bw Jaffari Matundu (wa tatu kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bi Zainabu Telack (wa tatu kulia) na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim Bw Stanley Kafu (wa pili kushoto)

LINDI; Oktoba 26, 2021: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, hii amezindua rasmi kampeni ya ugawaji madawati 1000 yaliyofadhiliwa na Benki ya Exim Tanzania kwa ajili ya shule za msingi katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dodoma, Mtwara, Lindi, Mbeya, Mwanza na Tanga.

Hatua hiyo inalenga kuunga mkono jitihada za serikali katika kukabiliana na uhaba wa madawati katika baadhi ya shule hapa nchini sambamba na kuboresha sekta ya elimu.

Hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo imefanyika Mkoani Lindi mapema jana na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi waandamizi wa serikali, baadhi ya wabunge wa mkoa wa Lindi, wananchi, wanafunzi pamoja na viongozi wa benki hiyo.

Akizungumza jana katika Uzinduzi huo Waziri Mkuu Majaliwa alisema pamoja na kuipongeza benki hiyo kwa jitihada hizo alisema hatua hiyio itasaidia sana katika kupinguza idadi ya wanafunzi wanaokabiliwa na chjangamoto ya ukosefu wa madawati huku akibainisha kuwa kwasasa serikali inaendelea na jitihada mbalimbali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuimaliza kabisa changamoto hiyo.

“Jitihada hizi za Benki ya Exim zimekuja wakati muafaka wakati pia serikali inaendelea kutoa fedha kwa ajili ya elimu katika kujenga vyumba vya Madarasa Nchini na kuboresha Miundombinu ya elimu Nchini.Lengo ni kuhakikisha kwamba pamoja na ongezeko hili la wanafunzi kutokana na mpango wa elimu lakini wanaketi kwenye madawati,’’ alisema Waziri Mkuu Majaliwa

Katika hafla hiyo ilishuhudiwa Waziri Mkuu Majaliwa akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bi Zainab Telack Madawati 200 kwa ajili ya Mkoa wa huo ikiwa ni sehemu ya mpango huo huku akiwaomba wadau mbalimbali kuiga mfano wa benki ya Exim kwa kujitokeza kwa wingi kuunga mkono jitihada hizo.

Awali akizungumza kuhusu kampeni hiyo Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bw Jaffari Matundu alisema ni mwendelezo wa mkakati wa benki hiyo katika kusaidia jamii unaofahamika kama Exim Cares na dhamira ya benki hiyo katika kuisaidia serikali kukabiliana na upungufu wa madawati katika baadhi ya shule hapa nchini.

“Uzinduzi wa kampeni hii muhimu unalenga kuunga juhudi za Serikali kuboresha miundo mbinu ya elimu hapa nchini. Kampeni itahusisha utoaji wa madawati 1000 katika mikoa mbalimbali hapa nchini Dodoma, Mtwara, Lindi, Mbeya na Mwanza na ugawaji wake utazingatia hali ya uhitaji,’’ alisema Bw Matundu katika taarifa yake mbele ya Waziri Mkuu Majaliwa.

“Kama ambavyo benki ya Exim tumejizatiti kutanua huduma zetu katika mikoa mbalimbali hapa nchini ndivyo ambavyo pia tumejipanga kuhakikisha kwamba uwepo wetu kwenye maeneo hayo unakwenda sambamba na uchangiaji wa huduma za kijamii ikiwemo elimu, afya na uhifadhi wa mazingira ambapo mwezi katikati ya mwaka huu tulishirikiana na Waziri Mkuu Mstaafu Mh Mizengo Pinda katika kufanikisha kampeni ya upandaji miti zaidi ya10,000 katika eneo la Zuzu jijini Dodoma,’’. Aliongezea.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bi Zainabu Telack aliishukuru benki hiyo kwa msaada huo huku akiiomba iendelee kutazama pia sekta nyingine ikiwemo afya.

“Nimefurahi kusikia kwamba mkakati wa benki ya Exim katika kupanua huduma zake zake katika maeneo mbalimbaliunakwenda sambamba na upanuzi wa mkakati wake katika kusaidia jamii. Huu ni mfano wa kuigwa na ni matarajio yangu kwamba kupitia jitihada kama hizi pia wananchi wa Lindi wataendelea

No comments: