Akizungumza
katika eneo la mradi, Bi, Nasombe amesema endapo mvua za vuli
zitanyesha kabla mfereji mkuu wenye urefu wa mita ELFU TATU NA MIANNE
(Mita3,400) kusakafiwa athari kubwa zinaweza kujitokeza ikiwemo maji
kubadili mwelekeo na kuvamia makazi ya watu kwa sababu ya mlundikano wa
udongo uliochimbwa kwaajili ya ujenzi wa Mfereji Mkuu unaoweza pia
kufukiwa kutokana na mvua zinazotarajiwa kunyesha hivi karibuni.
Kwa
upande wake Mhandisi Juma Hamsini wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji
amemshauri mkandarasi kuwashirikisha Wataalam wa Halmashauri, wanakijiji
wa Kirya na viongozi wa maeneo mradi unapotekelezwa kwa kuwa wanaijua
Geografia ya eneo husika na mazingira yanayowazunguka, suala
litakalomsaidia mkandarasi katika kutekeleza wajibu wake wakati huu wa
ujenzi.
Mnufaika
wa Mradi huo ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya ujenzi Bw, Nyange Laizer
ameishukuru serikali kwa mradi huo utakaoboresha maisha ya wafugaji
katika kijiji cha Kirya kwa kuongeza pato la familia kupitia kilimo cha
Umwagiliaji.
Mhandisi
Msimamizi wa Mradi huo kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Romwald
Robert, amekiri mkandarasi kuwa nyuma ya muda uliopangwa kwa mujibu wa
mkataba ambapo ameahidi kumsimamia kwa karibu mkandarasi huyo na
kumshauri ili aweze kutekeleza majukumu yake kwa kasi na kufidia muda
ulipotea hatimaye mradi huo ukamilike katika muda uliopangwa.
Ujenzi
wa Mfereji Mkuu utawezesha Banio la pili kuanza kufanya kazi na
kuongeza eneo la Umwagiliaji kutoka Hekta Mia nne Hamsini (Hekta 450)
hadi Hekta Miatisa (Hekta 900) ambapo ujenzi huo unajumuisha barabara
yenye urefu wa kilometa 16, vivuko viwili vya Miguu pamoja na Makalavati
na unatarajiwa kumalizika katika kipindi cha miezi 8 kwa gharama ya
zaidi ya Shillingi Bilioni Moja.
Skimu ya Umwagiliaji ya Kirya ina zaidi ya wanufaika Elfu mbili (2000) wanaolima zao la mpunga na Mbogamboga.
Mashine aina ya EXCAVATOR ikichimba Mfereji Mkuu unaotoa Maji kwenye Banio hadi katika Skimu ya Kirya.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Mwanga Bi, Mwajuma Nasombe (aliyevaa Miwani) akitoa
maelekezo kwa Bw, Nyange Laizer mjumbe wa kamati ya Ujenzi kuhusu wajibu
wa jamii ya Kirya kutoa ushirikiano unaohitajika kwa Mkandarasi.
Wahandisi
na Wataalam wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji wakitazama Banio la pili
litakaloanza kutumika mara baada ya Mfereji Mkuu kukamilika.
No comments:
Post a Comment