ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, November 10, 2021

SERIKALI YATOA NDEGE KWA STARS KUIFUATA MADAGASCAR

KATIKA kuweka mkazo wa kufuzu kombe la Dunia nchini Qatar 2022, Serikali ya Jamhuri wa Muungano Tanzania imetoa ndege ‘Air Bus’ kwa ajili ya mchezo wa Stars dhidi ya Madagascar.

Stars itakuwa na kibarua dhidi ya Madagascar mchezo utakaopigwa Novemba 14 baada ya kumaliza kucheza na DR Congo Novemba 11.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Katibu mkuu wa Wizara ya utamaduni, sanaa na michezo, Dk Hassan Abas amesema Serikali itatoa ndege kwa ajili ya mchezo huo ikiwa ni mkazo wa kuhakikisha timu inafanya vizuri.

“Labda tu niwaambie Serikali katika kuhakikisha tunasapoti michezo tutatoa ndege ya kwenda na kurudi kwa ajili ya mchezo huo, ndege hiyo itabeba wachezaji na benchi lote la ufundi, viongozi, wadau wa soka na waandishi wa habari kwa lengo la kwenda kuhabarisha watanzania”. ,” amesema Abas

Naye Katibu mkuu wa TFF, Wilfred Kidao amesema tayari wameshaanza maandalizi ya mchezo wao ujao dhidi ya Madagascar.

“Tayari tumeshaanza maandalizi ya mchezo wetu ujao dhidi ya Madagascar, lengo ni kuhakikisha tunapata ushindi”.

Stars inaongoza kundi J ikiwa na pointi 7 sawa na Benin huku nafasi ya tatu ikishikiliwa na DR Congo wenye pointi 5.

Mwanaspoti

No comments: