Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama,akizungumza wakati wa uzinduzi wa nembo na kaulimbiu ya maadhimisho ya sherehe ya miaka 60 ya Uhuru uzinduzi huo umefanyika leo November 1,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi, Dkt. Khalid Mohammed Salum,akizungumza wakati wa uzinduzi wa nembo na kaulimbiu ya maadhimisho ya sherehe ya miaka 60 ya Uhuru leo November 1,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya viongozi na waandishi wa habari wakifatilia hotuba mbalimbali wakati wa uzinduzi wa nembo na kaulimbiu ya maadhimisho ya sherehe ya miaka 60 ya Uhuru uzinduzi huo umefanyika leo November 1,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama,akizindua rasmi nembo na kaulimbiu ya maadhimisho ya sherehe ya miaka 60 ya Uhuru uzinduzi huo umefanyika leo November 1,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama,akiwa katika picha ya pamoja mara baada kuzindua nembo na kaulimbiu ya maadhimisho ya sherehe ya miaka 60 ya Uhuru uzinduzi huo umefanyika leo November 1,2021 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna,Dodoma
SERIKALI imezindua rasmi nembo na kaulimbiu ya maadhimisho ya sherehe ya miaka 60, ya Uhuru wa Tanzania bara zitakazofanyika Disemba 9, mwaka huu katika uwanja wa Uhuru mkoani Dar es Saalam.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo,Novemba mosi 2021,Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu Sera, Uratibu, Kazi, Vijana na Ajira Jenista Mhagama,amesema kutokana na umuhimu wa maadhimisho hayo mwaka huu serikali imeazimia kuwa na shughuli zitakazofanyika maeneo mbalimbali ya nchi.
“Lengo ni kutafakari kwa pamoja na kukumbuka tulikotoka, tulipo na tunakoelekea na hasa mafanikio tuliyopata yanayoonyesha dhahiri maendeleo ya miaka 60, ya uhuru wa nchi yetu na watu wake,”amesema.
Amesema shughuli za maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru zitahusisha Wizara na Taasisi zote za serikali kuelezea hatua ambazo kila sekta imepiga tangu Uhuru, tuliposasa na tunapoelekea.
Waziri huyo amesema ratiba ya mikutano ya Mawaziri na vyombo vya habari kuhusu historia ya nchi tangu ilipotoka uhuru hadi sasa kwa kila sekta itaanza Novemba 2, Novemba 2021,ambapo amedai mikutano hiyo inaratibiwa na Idara ya Habari – MAELEZO kwa kushirikiana na sekta husika 2021.
Pia amesema kutakuwa na mahojiano maalum kati ya vyombo vya habari na viongozi mbalimbali wa serikali walioko madarakani na wastaafu, watu mashuhuri, sekta binafsi na wananchi.
Amesema Mahojiano hayo yatahusisha viongozi na wananchi kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.
Vilevile amesema maadhimisho hayo yatahusisha mashindano ya insha kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, michezo kama mpira wa miguu, kikapu, wavu, riadha na mashindano ya baiskeli.
Pia kutakuwepo na maonyesho ya sanaa na ngoma za jadi, Makongamano ya Kikanda na Kitaifa, Mdahalo wa kitaifa, Maonesho ya Maalum ya Vijana kuonesha Ubunifu na ujuzi katika sekta mbalimbali pamoja na Maonesho ya Biashara ya Kitaifa yatakayotanguliwa na Mkutano wa uwekezaji.
Amesema matukio hayo yatafanyika katika Mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar kuanzia leo hadi Novemba 30, 2021.
Amesema Disemba 2, 2021 utafanyika uzinduzi rasmi wa Juma la Kilele cha sherehe za miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
“Uzinduzi huu utafanyika Jijini Dodoma na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”amesema
Amesema kuwa pia kutakuwepo na uzinduzi wa miradi mbalimbali ya Maendeleo itakayozinduliwa na viongozi wa Kitaifa wakiwemo wa mihimili ya Bunge na Mahakama wakiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Amesema kutakuwa na mkutano wa uwekezaji ambao utafuatiwa na maonesho ya kitaifa ya biashara utakaojumuisha wafanyabiashara wa pande zote mbili za Muungano.
“Mkutano na Maonesho hayo yatafanyika Zanzibar kuanzia Disemba 3, 2021 na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mheshimiwa Dk. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi”amesema.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi, Dkt. Khalid Mohammed Salum amesema kuwa uhuru wa Tanganyika wa mwaka 1961 ndiyo baba wa muungano.
“Tunashukuru sana sisi Zanzibar tumehusishwa katika hili kwani Uhuru wa Tanganyiaka ndiyo baba wa Muungano wetu lakini pia na sisi tutahakikisha Januari tunaishirikisha vilivyo Tanzania bara katika maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi”amesema Dk. Salum
No comments:
Post a Comment