ANGALIA LIVE NEWS

Friday, June 30, 2023

DC TANGA ATOA NENO KWA WASTAAFU KUHUSU MATAPELI

MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akizungumza wakati akifungua Semina kwa Wanachama wanaotarajia kustaafu Jijini Tanga iliyoandaliwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)
MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akizungumza wakati akifungua Semina kwa Wanachama wanaotarajia kustaafu Jijini Tanga iliyoandaliwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)
Meneja wa Mafao wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Makao Makuu James Oigo akizungumza wakati wa semina hiyo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akifuatia na Meneja wa Pensheni wa NSSF Makao Makuu Nancy Mwangamilo na Afisa na kushoto ni Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Cosmas Kadeghe na wa kwanza kulia ni Afisa Mkuu wa Idara ya Matekelezo wa NSSF Mkoa wa Tanga Abubakari Mshangama
Meneja wa Mafao wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Makao Makuu James Oigo akizungumza wakati wa semina hiyo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akifuatia na Meneja wa Pensheni wa NSSF Makao Makuu Nancy Mwangamilo na Afisa na kushoto ni Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Cosmas Kadeghe na wa kwanza kulia ni Afisa Mkuu wa Idara ya Matekelezo wa NSSF Mkoa wa Tanga Abubakari Mshangama
Afisa Mkuu wa Idara ya Matekelezo wa NSSF Mkoa wa Tanga Abubakari Mshangama akizungumza wakati wa semina hiyo kushoto ni Meneja wa Pensheni wa NSSF Makao Makuu Nancy Mwangamilo akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa ,Meneja wa Mafao wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Makao Makuu James Oigo na Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Cosmas Kadeghe
Meneja wa Pensheni wa NSSF Makao Makuu Nancy Mwangamilo akisisitiza jambo wakati wa semina hiyo
Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali
Sehemu ya wanachama wanaotarajiwa kustaafu Jijini Tanga wakiwa kwenye semina hiyo
Sehemu ya wanachama wanaotarajiwa kustaafu Jijini Tanga wakiwa kwenye semina hiyo
Meneja wa Benki ya NMB tawi la Ngamiani Elizaberth Chawinga kulia akifuatilia semina hiyo
Picha ya Pamoja
Na Oscar Assenga, Tanga

MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa amefungua Semina kwa Wanachama wanaotarajia kustaafu Jijini Tanga iliyoandaliwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) huku akitoa wito kwa wastaafu hao kuhakikisha wanafanya uwekezaji mapema ikiwemo kuepukana na magenge ya matapeli

Mgandilwa aliyasema mwishoni mwa wiki wakati akifungua semina hiyo kwa wanachama wanaotarajiwa kustaafu Jijini Tanga iliyoandaliwa na mfuko ambapo pia aliwataka kuepukana na magenge ya matapeli ambao wanahaingaika kuwashawishi kufanya biashara ambazo mlengo wao ni kwenda kuwaibia

Alisema kwamba kuna tabia ambayo imeibuka kwamba wafanyakazi wanapokaribia kustaafu lipo genge la matapeli ambalo limekuwa likijitokeza na kuwashawishi kufanya biashara ambazo mwisho wa wiki zinapelekea kuwaibia fedha ambazo wanakuwa wamezipata kama mafao yao.

“Katika Jambo hilo niwaase wastaafu tuweni makini sana na watu wa namna hii maana tunaweza kujikuta tunapoteza fedha zetu na mwisho wa tukajuta hivyo niwaase katika kipindi cha kuelekea kustaafu ni vema tukaanza maandalizi ikiwemo uwekezaji wenye tija”Alisema Mkuu huyo wa wilaya.

“Niwapongeze NSSF kwa kazi nzuri changamoto zinazowakumba watu wanaokaribia kustaafu kuna watu ambao ni genge la matapeli wanahaingaika kuwashawishi kufanya biashara ambazo mlengo wake ni kwenda kuwaibia hivyo niwasihi hakikisheni mnakuwa makini na watu wa namna hii”Alisema

Mkuu huyo wa wilaya pia alitumia wasaa huo kuwaasa kuhakikisha wanafanya maandalizi ya kustaafu kabla ya muda wa kustaafu lakini pia ni vema kuendelea kukumbushana kuna biashara ambazo zinaibuka kwenye msimu wa watu wanapokuwa wakitaka kustaafu hivyo nitoe rai kwa wastaafu kuona umuhimu wa kuhifadhi fedha wanazozipata.

Alisema licha ya kuhifadhi fedha hizo ni vema wawekeze kwenye maeneo yenye tija kwenye fedha lakini wakumbuke kuchagua marafiki kwenye kipindi hicho kutokana na kwamba wakati huo wapo ambao wanaweza kuibuka wakiwa na nia mbaya.

Awali akizungumza wakati wa semina hiyo Meneja wa Mafao wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Makao Makuu James Oigo alisema kwamba semina hiyo ni muhimu kutokana na kwamba ni maandalizi ya kustaafu kwa wafanyakazi ambao wanatarajiwa kustaafu lengo kubwa kuwaandaa kueleza dhana nzima ya hifadhi ya Jamii nafasi ya mfuko wa (NSSF) katika maisha yao baada ya kustaafu.
Alisema pia na jinsi ambavyo wanatakiwa wajiandee kwa ajili ya kupata mafao yao na namna watakavyotumia mafao yao katika maisha yao baada ya kustaafu ikiwemo kuwaondolea hofu ambayo jamii inayofikiri hakuna maisha baada ya kustaafu.

Alisema kwamba wanataka kuwapa elimu na kuwajenga kisaikolojia kwamba maisha yapo na NSSF ina nafasi kubwa sana kwenye maisha yao kwa kila pensheni wanayoipata kila mwezi na elimu hiyo imekuwa ikitolewa kwa mikoa yote nchini .

Naye kwa upande wake Mwanachama Mstaafu wa Mfuko wa NSFF Mkoani Tanga Martha Kazala alisema kwamba wanaushukuru mfuko huo na kwamba wanapokea pensheni kila mwezi na haina matatizo yoyote.

Alisema kwenye ustaafu wake ana miaka saba na anafurahia maisha yake kwa sababu yanamsaidia katika maisha yao watu wanafikiria ukiajiriw ukitoka kazini wanadhani hakuna maisha yanayoendelea baada ya kustaafu maisha ni mazuri kubwa inatakiwa uwe mvumilivu wakati wa ajira ili uweze kufanikiwa kwenye masuala la ustaafu na malipo ya pensheni.

Hata hivyo aliwataka waajiriwa wanaotarajiwa kusfaafu wajipange ili wanapopata fedha wafanye maamuzi yaliyokuwa na busara ya mipangilio ikiwemo kuepukane na vishiwsihi sambamba na kufuata maelekezo ya mifuko ya hifadhi  za jamii ili waweze kuishi vema

No comments: