Advertisements

Friday, June 9, 2023

MANYARA, MARA ZANG'ARA UMITASHUMTA

Timu za Mikoa ya Manyara na Mara zimeongoza katika mchezo wa riadha kuruka chini Wasichana na Wavulana bada ya kuibuka washindi katika michezo iliyochezwa leo tarehe 08 Juni 2023 kwenye viwanja vya Shule ya Sekondri Wavulana Tabora.

Manyara iliongoza kwa upande wa Wavulanabaada ya Michael Kerai kufanikiwa kuruka kwa umbali wa Mita 5.38 akifuatiwa na Baraka Mgaya wa Arusha aliyeruka Mita 5.25, nafasi ya tatu ikienda kwa Daniel Michael wa Dar es salaam aliyeruka Mita 5.14.

Wengine waliofuatia ni George Busiga kutoka mkoa wa Shinyanga Mita 5.11, Emmnuel Mkama wa Mara Mita 5.00, Joseph Yohana Kilimanjaro Mita 4.98, George Mahela kutoka Tanga Mita 4.87 na Joshua Aloyce wa Dar es salaam Mita 4.80.

Kwa Upande wa Wasichana Nyambane Sule kutoka Mkoani Mara aliruka kwa Mita 4.28, akifuatiwa na Yuta Reuben wa Tabora Mita 4.27, na nafasi ya tatu kwenda Mkoa wa Lindi baada ya Sophia Baraka kuruka Mita 4.23.

Nafsi zingine zilienda Mikoa ya Mtwara ambapo Milembe Wiliam alitumia Mita 4.23, akifuatiwa na Aisha Rashidi wa Mwanza Mita 4.22, Salma shija kutoka sinyanga Mita 4.20, Mwasiti Rashidi wa Katavi Mita 4.13, na Theresi Marco wa Singida Mita 4.12.

Fainali za michezo mbalimbali ya riadha ikiwepo kuruka chini, kurusha tufe na mbio za urefu tofauti zinatarajiwa kuanza Alhamisi Tarehe 9 Juni 2023 kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Tabora Wavulana.

No comments: