ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, June 21, 2023

PSPTB YAADHIMISHI WIKI YA UTUMISHI WA UMMA PAMOJA NA WAGONJWA


Katibu wa Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Furaha John (wa kwanza kushoto) akiongozana na wageni kutoka Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB Godfred Mbanyi (mwenye suti) walipofika katika katika Hospitali ya  Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya msaada wa mashuka kwenye Wodi ya Watoto waliozaliwa kabla ya wakati (watoto njiti) pamoja na kushiriki chakula cha mchana na wagonjwa wa wodi hiyo ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza tarehe 16 hadi tarehe 23 June 2023.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) Godfred Mbanyi (mwenye suti) akikabidhi msaada wa mashuka kwa Daktari Bingwa wa Watoto kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Dkt. Halima Mohamed Kassim uliotolewa katika Wodi ya Watoto waliozaliwa kabla ya wakati (watoto njiti)  katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Wafanyakazi wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Bodi hiyo Godfred Mbanyi  pamoja na wafanyakazi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma wakiwa wameshika moja ya mashuka yaliyotolewa na PSPTB kwa ajili ya Wodi ya Watoto waliozaliwa kabla ya wakati (watoto njiti).
Daktari Bingwa wa Watoto kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Dkt. Halima Mohamed Kassim akitoa ufafanuzi kwa Wafanyakazi wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Bodi hiyo Godfred Mbanyi kuhusu huduma zinazotolewa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma hasa kwenye Wodi ya Watoto waliozaliwa kabla ya wakati (watoto njiti) .
Daktari Bingwa wa Watoto kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Dkt. Halima Mohamed Kassim akitoa ufafanuzi kwa Wafanyakazi wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Bodi hiyo Godfred Mbanyi kuhusu chumba MAALUM kinachotumika kulaza watoto waliozaliwa kabla ya wakati (watoto njiti) kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma 
Waginjwa wa Wodi ya Watoto waliozaliwa kabla ya wakati (watoto njiti) pamoja na wauguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma wakipata chakula kilichoandaliwa na Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) ikiwa ni kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma.
Wafanyakazi wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) wakiwa wamebeba msaada wa mashuka kwa ajili ya kukabidhi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) Godfred Mbanyi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu walivyoamua kutumia wiki ya Utumishi wa Umma kwa ajili ya kutoa msaada wa mashuka kwenye Wodi ya Watoto waliozaliwa kabla ya wakati (watoto njiti) pamoja na kushiriki chakula cha mchana na wagonjwa wa wodi hiyo ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma
Katibu wa Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Furaha John akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kutoa msaada wa mashuka kwenye Wodi ya Watoto waliozaliwa kabla ya wakati (watoto njiti) pamoja na kushiriki chakula cha mchana na wagonjwa wa wodi hiyo ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma
Daktari Bingwa wa Watoto kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Dkt. Halima Mohamed Kassim akizungumza na waandishi wa habari kuhusu msaada uliotolewa na PSPTB katika ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma
Muuguzi wa Wodi ya Watoto Wachanga kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Analwise Misonge akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna walivyopokea msaada mashuka kwenye Wodi ya Watoto waliozaliwa kabla ya wakati (watoto njiti)  katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imetoa msaada wa mashuka kwenye Wodi ya Watoto waliozaliwa kabla ya wakati (watoto njiti) pamoja na kushiriki chakula cha mchana na wagonjwa wa wodi hiyo ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) Godfred Mbanyi amesema Bodi hiyo iko kwenye maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza tarehe 16 hadi tarehe 23 June 2023 na wameona watumie wiki hii kwa kurudisha kwa jamii ambapo leo wameweza kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kutoa msaada.

Pia amesema Bodi hiyo imeongeza muda kwa siku ya Jumatatu hadi Ijumaa kutoa huduma kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni ambapo amewasisitiza wateja wote kutumia fursa ya wiki ya Utumishi wa Umma kwa kufika katika ofisi za Dodoma na Dar es Salaam kwa ajili ya kupatiwa kupatiwa huduma pamoja na utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Naye Katibu wa Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Furaha John ametoa shukrani kwa uongozi wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) kwa kuwapatia msaada wa mashuka katika Wodi ya Watoto waliozaliwa kabla ya wakati (watoto njiti) na kusisitiza kuwa wanawakaribisha tena endapo wanawiwa kurudisha kwa ajili ya kutoa msaada katika hosptali hiyo.

No comments: