Advertisements

Saturday, June 3, 2023

WAZIRI DKT. CHANA ATETA NA KATIBU MKUU CAF

 

Na Shamimu Nyaki


Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Pindi Chana  Juni, 2, 2023  amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika ( CAF) Bw. Veron Mosengo Omba jijini Algiers nchini Algeria.

Mazungumzo hayo pia yamehudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Algeria Meja Jenerali Mstaafu Mhe. Jacob Kingu pamoja na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu  Tanzania (TFF) Ndg. Wallace Karia, ambapo Mhe. Pindi amemshukuru kwa kupokea andiko (bid) la maombi ya Tanzania, Kenya na Uganda kuandaa kwa pamoja mashindano ya AFCON  mwaka 2027.

Mhe. Pindi pia amemuhakikishia Bw. Veron kuwa Tanzania imejipanga kuhakikisha inaandaa miundombinu ya kisasa yenye viwango vya Kimataifa kwa lengo la kukidhi vigezo vya CAF vya kuandaa mashindano hayo.

Bw. Veron ametumia nafasi hiyo kuipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuweka mazingira mazuri ya kufanyika kwa shughuli za michezo.


No comments: