Advertisements

Saturday, June 3, 2023

ZAIDI YA WATU 200 WAFARIKI KWENYE AJALI YA TRENI INDIA


Zaidi ya watu 200 wamefariki dunia na wengine wengi wamejeruhiwa baada ya treni mbili za abiria na moja ya mizigo kugongana huko nchini India.

Kwa uchache watu 230 wamefariki na wengine 900 kujeruhiwa ambapo vyombo vya habari vya Kimataifa vimeripoti kuwa ajali hiyo inayoelezewa kuwa ni mbaya zaidi katika historian ya ajali za treni nchi India imetokea Mei 2, 2023 katika Jimbo la Odisha .

Zaidi ya magari 200 ya kubeba wagonjwa yalipelekwa kwenye eneo la tukio katika Wilaya ya Balasore, amesema Katibu Mkuu wa Jimbo la Odisha Pradeep Jena.



No comments: