Mwenyeiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk. Samia Sululuhu Hassan akimpongeza na kumaribisha meza kuu Katibu Muu mpya wa CCM Balozi Mstaafu Dk. Emanuel John Nchimbi, baada ya kutawazwa kushia wadhifa huo, leo mjini Zanzibar.
Uiimbwa wimbo wa Chama Cha Mapinduzi kumlaki meza Kuu Balozi Emmanuel Nchimbi. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Rais Dk. Hussein Mwinyi na kulia ni Maamu Mwenyekiti wa CCM Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana.
Mwenyeiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk. Samia Sululuhu Hassan akiteta jambo na Katibu Muu mpya wa CCM Balozi Mstaafu Dk. Emanuel John Nchimbi, baada ya ueti meza kuu.
Maamu Mwenyekiti wa CCM Bara Kinana aizungumza baada ya Balozi Dk. Nchimbi kuchaguliwa kuwa Katibu Muu wa CCM.
Balozi Mstaafu Dk. Nchinbi akiwa mwenye tabasamu la uhakika baada ya kuchaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM, leo.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa kauli moja imemchagua Balozi Mstaafu Dk. Emmanuel John Nchimbi kuwa Katibu Mkuu wake, kuchuua nafasi ya Daniel Chongolo aliyejiuzulu hivi karibuni.
CCM, imemchagua Balozi Dk. Chimbi kupitia mchakato wa vikao vya Kamati Kuu Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM vilivyofanyika, Mjini Zanzibar, leo Januari 15, 2024.
Baada ya Kamati Kuu Maalum ya CCM upendeeza jina la Balozi Dk. Nchimbi na kuliwasilisha kwenye kikao cha NEC, Kikao hicho kililipokea na Wajumbe bila ufanya ajizi wakaridhia kwa kauli moja na kumchagua uwa Katibu Mkuu wa CCM.
Mapema NEC iliiongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Rais wa Zanzibar na Mwenyeiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa kuendelea kutekeleza kwa ufanisi Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 – 2025 kwa upande wa Zanzibar na kufanikisha Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Pia NEC imeimepongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kuendelea kutekeleza kwa ufanisi Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 – 2025.
Kikao hicho kilitanguliwa na Semina kwa Wajumbe wa NEC kuanzia tarehe 13 – 14 Januari, 2024 ambayo wajumbe walipewa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati na kuridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wake.
Miradi hiyo ni pamoja na Mradi wa Bwawa la Umeme wa Julius Nyerere (JHPP) na mipango ya kuboresha hali ya umeme Nchini, Mradi wa Reli ya “Standard Gauge Railway (SGR)”, Ujenzi wa daraja la John Pombe Magufuli (Kigongo – Busisi), Utekelezaji wa Ilani ya CCM, kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Hali ya Mashirika ya Umma Nchini na Mageuzi yanayohitajika.
Pia walipewa taarifa ya mambo mengine, iiwemo taarifa ya Maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji mwaka 2024 na Maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 47 ya Kuzaliwa kwa CCM.
No comments:
Post a Comment