Sunday, February 11, 2024

MSAFARA WA MAKONDA WAPATA AJALI MASASI



Msafara wa Katibu wa NEC Itikadi Uenezi na Mafunzo wa CCM Paul Makonda umepata ajali katika kijiji cha Sululu, wilaya ya Masasi mkoani Mtwara leo majira ya 9 alasiri ikihusisha zaidi ya magari 10 yaliyokuwepo katika msafara huo yakirejea jijini Dar es Salaam baada ya kusitishwa ziara yake kutokana na kifo cha Waziri Mstaafu Edward Lowasa kilichotokea hapo jana.
Taarifa zilizothibitishwa kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa watu wasiopungua 7 wamejeruhiwa na kukimbizwa katika hospital ya Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara na huku kukiwa hakuna kifo chochote. Hata hivyo hali ya Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu Paul Makonda iko salama


No comments: