Thursday, February 15, 2024

MWILI WA LOWASSA WAWASILI JIJINI ARUSHA


Mwili wa aliyewahi kuwa Waziri Mkuu Edward Ngoyai Lowasa ukitolewa katika uwanja wa Kimataifa KIA tayari kwa kusafirishwa kuelekea nyumbni kwake Monduli Mkoani Arusha ambapo maziko yatafanyika siku ya Jumamosi Februari 17,2024
Gari lililobeba Mwili wa Aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Ngoyai Lowasa likitoka katika uwanja wa Kimataifa Kia kuanza safari kuelekea Arusha kwaajili yakuagwa na wananchi waliosimama pembezoni mwa barabara.

Na.Vero Ignatus , Kilimanjaro
Viongozi mbalimbali Ngazi ya Taifa,Chama na mikoa jirani wamejitokeza katika Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa ajili ya kuupokea mwili wa aliyekuwa Waziri Mkuu mstaafu Edward Ngoyai Lowassa ambapo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Mkoa wa Arusha wakiongoza mapokezi hayo.

Akizungumza namna ambavyo wanamfahamu Hayati Lowassa kwa upande wake mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi katika Vyombo vya habari Tanzania (Jowuta) Mussa Juma amesema alikuwa kiongozi wa kwanza kuwa na mahusiano ya karibu na waandishi wa habari nchini

"Sisi kama wana habari tutamkumbuka tulikuwa tukipata changamoto ya kiafya alikuwa katibu sanana sisi kwani alikuwa na nchango mkubwa sanakwa wanahabari tanzania na ni pigo kwa tasnia kwasababu alikuwa mdai mkubwa"alisema

Amesema kuwa anakumbuka kulikuwa na mgogoro wa maji ziwa Victoria kutoa maji ili kusambaza mikoa ya jirani lakini yeye aliongoza ujumbe wa Tanzania wakati akiwa Waziri wa Maji kushughulikia changamoto hiyo hilo hatimaye mradi ulikubaliwa na maji yalikwenda mikoa ya jiranini

"Hayati Edward Ngoyai Lowasa aliweza kusafiri na idadi kubwa ya waandishi wa habari kuelekea nchini Misri ambapo aliweza kwenda na kishughulikia hatimaye maji yakaanza kusambazwa katika mikoa jirani"alisema Musa

Amesema kuwa jambo jengine ambalo hatoweza kulisahau ni Ajenda tatu na kauli mbiu yake haswa katika wilaya ya Monduli kwani ilikuwa nyuma kimaendeleo ambazo zilikuwa ya kwanza ilikuwa Elimu, ya pili Elimu ya tatu Elimu haswa kwa watato wa kike katika masuala ya elimu haswa katika masuala ya elimu

Vilevile Hayati Edward Ngoyai Lowasa tunajifunza na kukumbuka ni jambo oa Kisiasa alikuwa hana siasa za uadui hakuwahi kutukana ama chochote hata alipohamia katika chama vha upinzani chadema hakuwahi kuitukana CCM hakuwa na hila wala uadui hivyo ni mfano wa kuigwa katika majukwaa ya siasa.

jKwa upande wake Kada wa CCM Jumapili Kiula mkoa wa Arusha na jimbo la uchaguzi Arusha mjini amesema Lowasa namfahamu kwa uchapakazi wake wa kukijenga chama pia alikuwa hakubali kushindwa na alikuwa anatekeleza ilani

Sema.kazi ya Mungu haina makosa ila ingekuwa ni amri yangu

No comments: