ANGALIA LIVE NEWS

Friday, March 8, 2024

WCF YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA KWA CHAMA CHA WAFANYAKAZI WA SERIKALI NA AFYA TANZANIA

Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma (kulia), akikabidhi sehemu ya msaada wa vifaa tiba kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Bernard Maro, kwenye ofisi ndogo za makao makuu ya WCF jijini Dar es Salaam.

NA K-VIS BLOG/KHALFANS AID

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umekabidhi vifaa tiba kwa Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) Mkoa wa Dar es Salaam.

Akipokea vifaa hivyo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma, jijini Dar es Salaam Machi 4, 2024, Mwenyekiti wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Bernard Maro ameishukuru WCF kwa msaada huo ambao utasaidia juhudi za Serikali katika kuboresha utoaji huduma za afya.

Bw. Maro ameongeza kuwa wakati wote WCF imekuwa ni miongoni mwa taasisi za umma ambazo zimekuwa zikitenga sehemu ya ilichonacho kusaidia jamii kupitia sera ya kurudisha kwa jamii.

“Lakini pia katika utekelezaji wa Sheria yenu iliyoanzisha Mfuko, WCF imekuwa karibu sana na wananchi hasa wale wanaopaswa kupata huduma mnazotoa,” amesema Bw. Maro na kuongeza kuwa kwa mujibu wa takwimu za TUGHE ambayo ina jukumu la kusimamia watumishi wa Serikali na Sekta ya Afya kutoka taasisi za Umma na Binafsi, WCF imekuwa ikitekeleza kwa vitendo masuala ya Utawala Bora, Huduma Bora na Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Wateja wa Mfuko.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma, alisema, Mfuko umekuwa na ushirikiano mzuri na chama cha TUGHE tawi la WCF, “Hili lazima niliseme mapema bila ya kusubiri ‘forum’ nyingine, TUGHE tawi wamekuwa na mchango mkubwa wa kutuletea mawazo ya kuboresha na kuimarisha taasisi yetu, wamekuwa ni watu wanaoongeza busara badala ya kuchochea moto pale panapokuwa na viashiria vinavyohitaji majadiliano” amefafanua

Aidha Dkt. Mduma amebainisha kuwa ushirikiano kama huo umekuwepo kwa kuwa wanaamini kuwa chama hicho ni chombo muhimu cha kuusaidia Mfuko katika ngazi za mkoa na taifa ikiwa ni pamoja na kuwawezesha wadau wa Mfuko kuelewa huduma zinazotolewa pamoja na haki zao.

“Kuhusu siku hii ya Wanawake Duniani, WCF imeamua kuwaunga mkono TUGHE ili kufikisha mahitaji muhimu kwa makundi mbalimbali yaliyoainishwa wakati huu wa maadhimisho ya siku Wanawake Duniani.” Alisema Dkt. Mduma.

Siku ya Wanawake Duniani huadhimishwa tarehe 8 Machi ya kila mwaka.

No comments: