ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, April 13, 2024

KINANA AWASILI MARA, KUANZA ZIARA YA KUIMARISHA CHAMA.


Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana, amewasili mkoani Mara kwa ziara ya kuimarisha Chama.

Kinana amepokelewa leo April 13, 2024 katika Kijiji cha Ikoma, Wilaya ya Serengeti mkoani Mara ambapo mapokezi hayo yaliongozwa na Kaimu Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa huo, Christopher Gachuma.
Akizungumza katika mapokezi hayo Kinana amewashukiru wana CCM na wananchi kwa ujumla kwa kuendelea kukiunga mkongo Chama na serikali.

Kwa upande wake Gachuma alimpongeza na kumkaribisha Kinana mkoani humo.

No comments: