Friday, May 24, 2024

WANANCHI WA KAGERA, SINGIDA WAFIKIWA NA ELIMU YA FEDHA


Afisa Usimamizi wa Fedha, kutoka Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Salim Kimaro, akitoa elimu ya fedha kwa wajasiriamali na wananchi wa Halmashauri ya Ikungi, mkoani Singida, Kama sehemu ya utekelezaji wa mpango wa Wizara ya Fedha wa kutoa elimu ya fedha vijijini ili kuwapa uelewa wananchi kupata uelewa kuhusu usimamizi wa fedha binafsi, masuala ya mikopo, na kuweka akiba.
Afisa Usimamizi wa Fedha Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya, akifafanua jambo wakati wa semina ya utoaji elimu kwa wananchi iliyofanyika katika Ukumbi wa Kashura “Women Centre” uliopo katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.
Afisa Usimamizi wa Fedha Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya, akimkabidhi vipeperushi vyenye taarifa mbalimbali kuhusu elimu ya fedha Bi. Ivona Gasper baada ya kumalizika kwa semina ya utoaji elimu kwa wananchi iliyofanyika katika Ukumbi wa Kashura “Women Centre” uliopo katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.
Afisa Usimamizi wa Fedha Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya, akizungumza wakati wa semina ya utoaji elimu kwa wananchi iliyofanyika katika Ukumbi wa Kashura “Women Centre” uliopo katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.

Baadhi ya wananchi walioshiriki semina ya elimu ya fedha wakifuatilia makala yenye mada mbalimbali ikiwemo utunzaji wa akiba, mikopo, maandalizi ya kustaafu na nyinginezo iliyofanyika katika Ukumbi wa Kashura “Women Centre” uliopo katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.
Baadhi ya wananchi walioshiriki semina ya elimu ya fedha wakiangalia makala yenye mada mbalimbali ikiwemo utunzaji wa akiba, mikopo, maandalizi ya kustaafu na nyinginezo iliyofanyika katika Ukumbi wa Kashura “Women Centre” uliopo katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera

SINGIDA
Afisa Usimamizi wa Fedha, kutoka Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Elizabeth Mnzava akitoa elimu ya fedha kwa wajasiriamali na wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ikungi Mkoani Singida, katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo, ili kuhakikisha kuwa wananchi hao wanakuwa na matumizi sahihi ya fedha binafsi, kufahamu mambo ya kuzingatia kabla ya kuomba mikopo, na kuepukana na madhara ya mikopo umiza.
Baadhi ya wajasiriamali na Wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ikungu, Mkoani Singida, wakifuatilia mafunzo ya elimu ya fedha katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo, kwa njia ya filamu zenye maudhui mbalimbali ikiwemo madhara ya kukopa bila malengo, madhara ya kukopa sehemu ambazo hazijasajiliwa, kuweka fedha kwenye vikundi ambavyo havijasajiliwa, matumizi mabaya ya fedha binafsi na mambo ya kuzingatia kabla ya kukopa fedha, mafunzo hayo yameandaliwa na kutolewa na Wizara ya Fedha.
Mratibu wa huduma ndogo za fedha katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Bw. Peter Musa ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii, akitoa elimu kwa wajasiriamali, wafanyabiashara na wananchi mbalimbali waliohudhuria katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Ikungi kupata elimu ya fedha kuhusu usajili wa vikundi.
Mratibu wa huduma ndogo za fedha katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Bw. Peter Musa ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii, akitoa elimu kwa wajasiriamali, wafanyabiashara na wananchi mbalimbali waliohudhuria katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Ikungi kupata elimu ya fedha kuhusu usajili wa vikundi.

Na Josephine Majula, WF- Kagera
Wananchi wa Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kupitia Wizara ya Fedha kwa kuwafikishia huduma ya elimu ya fedha itakayowakomboa kiuchumi na kuwaepusha na upotevu wa fedha.

Shukrani hizo zimetolewa na wananchi hao baada ya kumalizika kwa semina ya elimu ya fedha iliyotolewa na Wizara ya Fedha kupitia Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha iliyofanyika katika Ukumbi wa Kashura “Women Centre” uliopo katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya kupata elimu hiyo, Bi. Ivona Gasper Mfanyabiashara alisema kuwa elimu aliyoipata ataenda kuwaelimsha wengine ili waweze kuwa na uelewa mpana wa masuala ya fedha.

“Tunaiomba Serikali iendelee kutoa elimu ya fedha kwa wananchi wake na kuhakikisha inawafikia watu wote nchi nzima kwa sababu wananchi wengi wanapoteza fedha kwa kukosa elimu” alisema Bi. Gasper.

Mwelimishaji Rika Ngazi ya Jamii Bi. Jackline Petro, alisema kuwa baada ya kupata elimu ya fedha amejua sehemu sahihi ya kutunza fedha zake kama vile benki, saccoss mbalimbali na vikundi vidogo vidogo vilivyosajiliwa.

Naye Afisa Usimamizi wa Fedha Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya, alisema kuwa Serikali itahakikisha watu wote waliokusudiwa kupata elimu awamu ya kwanza wanafikiwa kama ilivyopangwa.

“Tumejipanga kutoa elimu kwa watu wote, watoa huduma na watumiaji huduma za fedha ili wawe na uelewa wa pamoja na mambo ya kuzingatiwa kuhusani wakati wa kutoa mikopo au kuchukua mikopo” alisema Bw. Kibakaya.

Kwa upande wake Afisa Biashara Mkoa wa Kagera na Mratibu wa Huduma za Fedha ngazi ya Mkoa, Bw. Keneth Mlilo, alisema kuwa kumekuwa na mwitikio mkubwa kwa wananchi kujitokeza kupata elimu ya fedha hususan kundi la kinamama kwa kuwa imeonekana kundi hilo ndilo waathirika wakubwa wa mikopo umiza yenye riba zisizolipika

No comments: