Tuesday, June 11, 2024

ACT WAZALENDO WAFANYA MKUTANO WA HADHARA UNGUJA


Mjumbe wa Kamati Kuu Chama cha ACT Wazalendo Mansour Yussuf Himid amesema kuna umuhimu mkubwa kuendelea harakati za kudai mabadiliko ya uongozi Zanzibar kwani chama kinachoendelea kutawala sasa hakina dhamira njema kwa wananchi wa Zanzibar bali wapo kwa ajili maslahi yao binafsi.
Mansour ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uwanja wa kivumbi Shehia ya Kwamtipura, Jimbo la Shauri Moyo Mjini Unguja.

Amesema kuna umuhimu mkubwa kwa wananchi wa Zanzibar kuendelea kushikamana bila kujali maslahi ya chama na badala yake wakichague chama cha ACT Wazalendo ili kiongoze Zanzibar kwa misingi ya kisheria na matakwa ya walio wengi.

Amesema kwa muda wote wa utawala wa Chama cha Mapinduzi awamu hii inayoongozwa na Dkt, Hussein Ali Mwinyi imekithiri rushwa na uhujumu wa uchumi huku wanaofanya hayo wakishindwa kuchukuliwa hatua yoyote hile.

Amesema kwa sababu ya kukosa misingi imara ya uongozi kwenye chama hicho CCM wameamua kuwawekea chuki wale wote wasiokiunga chama chao na kuwakosehs ahaki za msingi zikiwemo za kupata vitambulisho pamoja na nafasi za ajira.

‘’Hii ni dalili mbaya sana ukiona kiongozi anaogopwa kusemwa maana yake hana uadilifu na lazima wajue wazee wetu wamepindua ili tuishi kwa upendo na mshikamano sio wanavotufanya wao tuishi’’alisema Himid.
Sambamba na hayo alisema wazanzibar wanapaswa kufahamu kuwa Chama cha Mapinduzi CCM hakijawahi kushinda Uchaguzi hata mmoja Zanzibar awamu zote na kueleza kuwa chini ya Rais Mwinyi ACT wazalendo itashinda kirahisi mnoo.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Zanzibar Ismail Jussa Ladhu amesema wataendelea kufanya kazi za siasa wakiamini kuwa wananchi wa Zanzibar wamechoshwa na ugumu wa maisha uliosababishwa na CCM.

Pia Jussa ameshangazwa na viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM kuendelea kuhubiri vitisho kwenye mikutano yao na kueleza kuwa kufanya hivyo ni kuishiwa sera na ndio maana wanahubiri chuki na sio kufanya kazi za siasa.

“Wacheni kufanya vitisho kwa wananchi watu washawakataeni na nilazima 2025 tuwaondoe kwa nguvu ya wananchi” alieleza Jussa.

Ameeleza na mipango mibovu ya Serikali inayoongozwa na CCM leo wafanyakazi wote ambao ni waajiriwa wana hali duni sana ya maisha.

Amefahamisha kuwa kwa sababu ya mazingira hayo imefika wakati waajiriwa wa Serikali wanawekeza malengo yao kwenye pesa ambazo watalipwa baada ya kustaafu kazi wakati ambao hawana nguvu tena ya kufanya lolote na baada ya muda mfupi hufariki Dunia kwa sababu ya msongo wa mawazo.

Alisema kutokana na utawala huu ambao haujali maslahi ya wananchi inasikitisha sana katika tawala zote zilizowahi kupita, Zanzibar haijawahi kuwa na deni kubwa zaidi kuliko awamu hii inayoongozwa na Dkt,Hussein Ali Mwinyi na kwamba kwa kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake hadi sasa Zanzibar inadaiwa shilini trilioni 1.1 kiasia ambacho hakijawahi kutokea kwa awamu zote.

Alisema Serikali iliyopo madarakani imekuwa ikikopa mpaka benk za ndani na kupelekea kudai kila pembe ya Dunia.

Alisema kiwango hichi kikubwa cha deni ni kukosekana kwa misingi bora ya uongozi pamoja na ufisadi mkubwa unaofanywa kila leo huku wanaofanya licha ya kutajwa kwao katika ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Seriukali (CAG) hakuna kinachofanyika kwa wanaotenda hayo wakishindwa kuwajibishwa.

Awali akizungumza kwenye mkutano huo mjumbe wa Kamati Kuu Shuena Faki Haji amesema kuwa kwa muda mrefu Wananchi wa Zanzibar wamekuwa wakibaguliwa kwa itikadi za kisiasa jambo ambalo limewarudisha nyuma kimaendeleo.
Alieleza kuwa kwa sababu watawala waliopo madarakani wamekuwa wakijali sana matumbo yao na familia zao huku wakiwacha wengine katika hali ngumu za kimaisha.

No comments: