Sunday, July 21, 2024

RAIS JOE BIDEN AJITOA KWENYE MBIO ZA URAIS

Rais wa Marekani Mhe. Joe Biden (pichani) amejitoa kwenye mbio za urais ambazo ulikuwa ufanyike mwezi Novemba mwaka huu na badala yake amempendekeza makamu wake wa urais wake. Mhe. Kamala Harris. Uamuzi huo umepongezwa na wengi na kuita uamuzi huo kuwa ni wa kizalendo na wenye nia na mapenzi mema kwa nchi yake.

Uamuzi huo umewashtuwa wengi kutokana na hotuba yake ya kampeni wiki iliyopita aliposema yeye haendi kokote, Chama chake cha Democratic kiliingiwa na wasiwasi baada ya Rais Joe Biden kutofanya vizuri kwenye mdahalo wa urais uliofanyika mwezi uliopita.

Wachambuzi wa maswala ya siasa wamesema kujitoa kwake kutawapa upande wa pili wakati mgumu kidogo kutokana kwamba walishapanga mipango ya kumzungumzia Rais Jeo Biden badala ya makamu wa Rais.

No comments: