Thursday, August 29, 2024

RAIS SAMIA AKABIDHI JWTZ NDEGE ZA MAFUNZO YA AWALI YA URUBANI NA MABASI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria kuzindua na kukabidhi ndege za mafunzo ya awali ya Marubani na mabasi ya usafirishaji kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwenye hafla iliyofanyika katika Kikosi cha Usafirishaji Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Agosti, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishuka kwenye moja ya mabasi ya usafirishaji mara baada ya hafla ya kuyakabidhi kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika hafla iliyofanyika katika Kikosi cha Usafirishaji Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Agosti, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na Viongozi wengine wakati Wimbo wa Taifa ukiimbwa kabla ya hafla fupi ya uzinduzi na kukabidhi ndege za mafunzo ya awali ya Marubani na mabasi ya usafirishaji kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika hafla iliyofanyika katika Kikosi cha Usafirishaji Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Agosti, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Maafisa na Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakati wa hafla ya uzinduzi na kukabidhi ndege za mafunzo ya awali ya Marubani na mabasi ya usafirishaji kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika hafla iliyofanyika katika Kikosi cha Usafirishaji Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Agosti, 2024.








No comments: