Wednesday, August 28, 2024

RAIS WA ZANZIBAR DKT.HUSSEIN MWINYI AJUMUKA KATIKA MAZIKO YA MAREHEMU MVITA MUSSA KIBENDERA

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Wananchi katika Sala ya Maiti kumsalia marehemu Mvita Mussa Kibendera, iliyoongozwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi, iliyofanyika katika Masjid Mushawar Muembeshauri Wilaya ya Mjini Unguja leo 27-8-2024.(kulia kwa Rais) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Alhajj Othman Masoud Othman na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Khamis Abdalla Ramadhan na (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla,Spika wa Baraza la Wawakilishi.Alhajj Zuberi Ali Maulid na Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhajj Dkt.Amani Karume. (Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Wananchi katika kuitikia dua ya kumuombea Marehemu Mvita Mussa Kibendera ,baada ya kumalizika kwa Sala ya Maiti, ikisomwa na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Hassan Othman Ngwali,iliyofanyika katika Masjid Mushawar Muembeshauri Wilaya ya Mjini Unguja leo 27-8-2024.(kulia kwa Rais) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Alhajj Othman Masoud Othman na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Khamis Abdalla Ramadhan na (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla,Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.Alhajj Zuberi Ali Maulid na Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhajj Dkt.Amani Abeid Karume. (Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiweka mchanga katika kaburi la marehemu Mvita Mussa Kibendera, wakati wa maziko yake yaliyofanyika katika makaburi ya Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 27-8-2024.(Picha na Ikulu)

No comments: