ANGALIA LIVE NEWS

Friday, August 9, 2024

SIMBACHAWENE ANENA AJIRA MPYA KWA WALIMU NA MADAKTARI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mbunge wa Jimbo la Kibakwe Mhe. George Simbachawene akizungumza na wananchi wa Kata ya Wangi Jimbo la Kibakwe kwenye mkutano wa hadhara alipokuwa akiongea na wananchi na kuzindua Shule ya Sekondari Wangi.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Wangi wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mbunge wa Jimbo la Kibakwe Mhe. George Simbachawene wakati wa uzinduzi wa Shule hiyo katika Jimbo la Kibakwe.

“Ninamuelekeza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, kushirikiana na Katibu Mkuu TAMISEMI ili kuhakikisha shule zote mpya na vituo vya afya nchi nzima vilivyokamilika vinapangiwa Walimu na Madaktari mtawalia”.

Maelekezo hayo yametolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mbunge wa Jimbo la Kibakwe Mhe. George Simbachawene Agosti 7, 2024 wakati alipokuwa akiongea na wananchi wa Kata ya Wangi Jimbo la Kibakwe kwenye mkutano wa hadhara alipokuwa akiongea na wananchi na kuzindua Shule ya Sekondari Wangi.

“Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa ajira zaidi ya elfu 12 kwa sekta ya afya na nyingine kwa sekta ya elimu, hivyo hatuna budi kuhakikisha wanapangwa vizuri ili wananchi wapate huduma ipasavyo” alisema Mhe. Simbachawene.

Aidha, Mhe. Simbachawene amewaomba wananchi wa Kata ya Wangi na Wotta kushukuru kwa maendeleo ambayo yameletwa na Rais Dkt. Samia mathalani ujenzi barabara, shule na vituo vya afya kwa lengo la kurahisisha maisha kwa Wananchi.

Hivyo, wananchi wameombwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kumpa kura za ndiyo Rais Mhe. Dkt. Samia, Mbunge Mhe. Simbachawene na Madiwani ili waenedelee kutekeleza maono waliyonayo badala ya kuanza upyya.

Mhe. Simbachawene anaendelea na ziara yake katika Jimbo la Kibakwe ambapo amefanya mikutano ya hadhara katika Kijiji cha Wotta na Wangi Jimbo la Kibakwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.

No comments: