ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, August 14, 2024

TGNP YATOA MAFUNZO KWA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA ILI KUONGEZA USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA NGAZI ZA UONGOZI NA MAAMUZI

Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijinsia Tanzania(TGNP), Liliani Liundi akisona hotuba kwa washiriki wakati wa ufunguzi wa warsha ya mafunzo kwa Viongozi wa vyama vya Siasa ili kuongeza ushiriki wa wanawake katika ngazi za uongozi na maamuzi  iliyofanyika katika ofisi zake zilizopo Mabibo jijini Dar es Salaam.

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Dorothy Semu akizungumza namna alivyiweza kuwa kiongozi mkubwa wa chama pamoja na changamoto alizozipitia wakati wa ufunguzi wa warsha ya mafunzo kwa Viongozi wa vyama vya Siasa ili kuongeza ushiriki wa wanawake katika ngazi za uongozi na maamuzi iliyofanyika katika ofisi zake zilizopo Mabibo jijini Dar es Salaam.
wenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chama cha demokrasia na maendeleo, (BAWACHA), Sharifa Suleiman akielezea kuhusu changamoto wanazozipitia Wanawake kwenye masuala ya uongozi wakati wa ufunguzi wa warsha ya mafunzo kwa Viongozi wa vyama vya Siasa ili kuongeza ushiriki wa wanawake katika ngazi za uongozi na maamuzi iliyofanyika katika ofisi zake zilizopo Mabibo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Chama cha Wananchi (CUF), ACT Wazalendo, Chama cha Kijamii (CCK) na NCCR Mageuzi wakifuatilia  ufunguzi pamoja na mada zilizokuwa zinatolewa wakati wa ufunguzi wa warsha ya mafunzo kwa Viongozi wa vyama vya Siasa ili kuongeza ushiriki wa wanawake katika ngazi za uongozi na maamuzi iliyofanyika katika ofisi zake zilizopo Mabibo jijini Dar es Salaam.
Mwezeshaji wa Mafunzo Deo Temba akiwasilisha mada kuhsus dhana za jinsia na ushiriki wa Wanawake katika uongozi kwa washiriki kutoka vyama vya siasa mbalimbali katika warsha ya mafunzo kwa Viongozi wa vyama vya Siasa ili kuongeza ushiriki wa wanawake katika ngazi za uongozi na maamuzi iliyofanyika katika ofisi zake zilizopo Mabibo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Chama cha Wananchi (CUF), ACT Wazalendo, Chama cha Kijamii (CCK) na NCCR Mageuzi wakichangia mada zilizokuwa zinatolewa wakati wa warsha ya mafunzo kwa Viongozi wa vyama vya Siasa ili kuongeza ushiriki wa wanawake katika ngazi za uongozi na maamuzi iliyofanyika katika ofisi zake zilizopo Mabibo jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja 


Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) imeanda mafunzo kwa Viongozi wa vyama vya Siasa ili kuongeza ushiriki wa wanawake katika ngazi za uongozi na maamuzi ambapo mafunzo hayo yamejumuhisha washiriki kutoka katika Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Chama cha Wananchi (CUF), ACT Wazalendo, Chama cha Kijamii (CCK) na NCCR Mageuzi.

Akizungumza wakati wa kufungua warsha hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Liliani Liundi amesema lengo kuu la warsha hiyo kuongeza ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi na ngazi za usimamizi ili kuongeza uelewa wa dhana ya jinsia na uongozi pamoja na kujenga uelewa wa pamoja kuhusu mifumo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa na fursa zilizopo katika kuwezesha wanawake wanashiriki kwnye nafasi za maamuzi.

Pia amesema wanaweka mikakati ya pamoja ya kuongeza ushiriki wa wanawake kwenye nafasi za uongozi kwenye kata husika pamoja na kuimarisha mahusiano na kujenga nguvu ya pamoja na kayoka kutekeleza ajenda ya usawa wa kijinsia katika siasa.

“Ushirikishwaji wa kisiasa unahitaji makundi yote ya watu ikiwemo wanaume na wanawake pamoja na makundi dhaifu bila kusahau kundi la walemavu ambalo limeachwa nyuma halihusishwi katika uongozi wa kisiasa na masuala ya uchaguzi” Alisema Liundi

Pia amewasisitiza washiriki wote wa mafunzo hayo kufahamu ilani za vyama vyote vya kisiasa ikiwemo tofauti zake na mahali pa kuboresha ili kuweza kujadili sera ya jinsia ndani ya vyama vya siasa .

Naye Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Dorothy Semu ameishukuru TGNP kwa kuweza kutoa fursa kwa wanasiasa wa vyamba mbalimbali vya siasa kuja kujifunza nasuala ya uongozi ili kuweza kuhimarika katika masuala ya kijinsia hasa kwenye uchaguzi uja wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Pia amewasisitiza washiriki kuwa wazalendo wa nchi yao kwasababu vyama vya siasa ni walinzi wa kuhakikisha wanawake wanahusika katika siasa pamoja na serikalini hasa kwa kupata nafasi kubwa za uongozi kwani wao wanaweza.

No comments: