Na Sophia Kingimali.
Taasisi ya Uhasibu nchini (TIA) inatarajia kuandika historia katika Mkoa wa Tanga kwa kufungua chuo kikuu(TIA campas) katika mkoa huo na kufanya kuwa chuo kikuu cha kwanza katika mkoa huo.
Akizungumza na waandishi wa habari Agost 7,2024 Jijini Dodoma kwenye maonesho ya Kimataifa ya wakulima,wavuvi na wafugaji Nanenane Afisa Mtendaji Mkuu Profesa William Pallangyo amesema kwa mwaka huu Taasisi hiyo inafungua tawi leo kubwa Tanga.
Amesema tawi ambalo wanategemea kulifungua kwamba litakua linafundisha wanafunzi kuanzia level ya cheti (basic certificate),Diploma (stashahada) pia watakuwa na shahada ya kwanza
“Kwenye ngazi hizo tutafundisha masomo yanayohusiana na uhasibu, procurement and logistics, human resource management, marketinga na public relations pamoja na public sector accounting, hayo ni maeneo tunayotegemea wananchi wa Tanga watafaidi kwa muda mfupi ujao”,Amesema na kuongeza
“Tumeona tutumie fursa hii pia kuwaambia wananchi wote popote walipo kwamba kuna campus mpya iliyopo Tanga na ni campus ambayo bahati nzuri pia ina hostel za wanafunzi kukaa”,Amesema.
Akizungumzia kampasi ya Singida prof.Pallangyo amesema Singida ni mji ambao umekua na taasisi za elimu ya juu lakini hauna nafasi ya kusoma shahada ya udhamiri (masters) lakini mwaka huu wamepata bahati, serikali imeturuhusu kuanzisha shahada za udhamiri katika campus hiyo ya Singida.
Sambamba na hayo amesema TIA imekua ikiona changamto ambazo wanafunzi wanazipata hasa za kulipia ada,Taasisi kwa kuliona hilo tarehe 26 mwezi wa 10 wanategemea kuwa na TIA MARATHON ambayo itaongozwa na Waziri wa fedha Dkt.Mwigulu Nchemba.
Amesema lengo la Marathoni hiyo ni kupata fedha ambazo zitadaidia wanafunzi.
“Kuna baadhi ya wanafunzi ambao wamepata bahati ya kusoma sekondari lakini wanapofika vyuo vikuu wanapata changamoto za kulipa ada, hivyo marathon yetu itakwenda kusaidia kwenye makundi makubwa mawili kundi la kwanza ni wale wanafunzi ambao hawana uwezo wa kifedha lakini kundi la pili tunawaita “young mothers” Wale wanafunzi ambao wamekuja chuoni lakini pia wana familia , wana watoto wadogo kwa hiyo ili ni kundi ambalo tumeona ni muhimu liweze kusaidiwa kuweza kusoma kwa furaha kwa maana ya kuwasaidia sehemu ya fedha ambazo watazihitaji”,
Sambamba na hiyo pia amesema wanatarajia mwaka huu kuwa mkutano unaoitwa Mkutano wa tatu(The third international conference on business studies) ambao utafanyika Arusha ambapo Kongamano hili tunategemea lifanyike kati ya tarehe 07 hadi tarehe 09 mwezi wa 11 hukub mgeni rasmi akitarajiwa kuwa awe ni naibu waziri mkuu na waziri wa nishati Doctor Biteko.
Kwa upande wao wanafunzi ambao ni wanufaika wa chuo hiko Yusuph Mtimandole aliyebuni mfumo wa kuuza korosho(CUSHENUTZ) Mtwara na Nicolaus Mboya aliyebuni mfumo (FARM CONNECT)wamepongeza juhudi zinazofanywa na chuo hiko katika kumsaidia mwanafunzi kutimiza wajibu na kuhakikisha anakuwa fursa kwa wengine na hatimae kuendelea kuzalisha ajira nyingi kwa vijana.
No comments:
Post a Comment