Thursday, September 12, 2024

DKT.DIMWA : ASEMA CCM ITAENDELEA KUFANYA SIASA ZA KISTAARABU PEMBA


NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa,akivishwa sikafu baada ya kuwasili katika Ofisi ya CCM Mkoa wa Kusini Pemba kwa ajili ya mwendelezo wa ziara ya Sekretarieti ya Kamati Maalum ya NEC,CCM Taifa Zanzibar.
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa,akishiriki ujenzi wa taifa na kukagua mradi wa frame ya duka katika Maskani ya CCM Bwegeza Jimbo la Kiwani Pemba.
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa,akizungumza na wanachama wa CCM Tawi la Kengeja Jimbo la Mtambile mara baada ya kukagua ujenzi wa tawi hilo katika ziara ya Sekretarieti ya Kamati Maalum ya NEC,CCM Taifa Zanzibar katika Wilaya ya Mkoa kichama Pemba.

NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa,amewataka Wanachama wa CCM waliotimiza umri wa miaka 18 kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika zoezi la awamu ya pili ya kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili wapate vitambulisho vya kupiga kura.

Kauli hiyo ameitoa wakati akiweka jiwe la msingi katika Tawi la CCM Ngwachani Jimbo la Chambani Wilaya ya Mkoani katika mwendelezo wa ziara yake ya kikazi ya Sekretarieti ya Kamati Maalum ya NEC,CCM Taifa Zanzibar Mkoa wa Kusini Pemba.

Dkt.Dimwa, aliwasihi Wanachama hao kuwa Wana wajibu wa kujiandikisha katika daftari hilo na kupata vitambulisho vya kupiga kura sambamba na kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kuwapigia kura za ndio wagombea wote wa CCM katika uchaguzi mkuu wa dola wa mwaka 2025.

Katika maelezo yake Dkt.Dimwa, alisema maendeleo endelevu ya kisiwa Cha Pemba yataendelea kuimarika endapo wanachama na Wananchi wa kisiwa cha Pemba wataichagua CCM kwa kura nyingi iendelee kuongoza dola katika uchaguzi mkuu ujao.

" Chama Cha Mapinduzi tumedhamiria kuhakikisha Pemba inapiga hatua kubwa za kimaendeleo na kuwa kituo kikuu cha kukuza Uchumi wa nchi.

Kupitia Ilani ya uchaguzi ya CCM tutaimarisha sekta zote za kiuchumi na kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na maisha bora na kipato Cha uhakika kinachoendana na hadhi ya Zanzibar Kitaifa,kikanda na kimataifa.",alieleza Dkt.Dimwa.

Kupitia ziara hiyo aliwakumbusha pia Wanachama wasiokuwa na vitambulisho vya mzanzibar mkaazi (ZANID) na wana sifa za kisheria kupata haki hiyo wahakikishe wanafuata utaratibu kupata vitambulisho hivyo.

Alisema Serikali ya awamu ya nane chini ya uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Mwinyi ameendelea kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025 kwa kuimarisha sekta za Elimu,afya,barabara za kisasa,ujenzi wa Bandari za kisasa,ujenzi wa Uwanja wa ndege wa kisasa,kujenga viwanda katika maeneo huru ya uwekezaji na kupandisha thamani ya mazao ya mwani na karafuu.

Kupitia ziara hiyo alisema Rais Dk.Mwinyi,amefanya mambo mengi ya maendeleo na kuvuka malengo ya Ilani pamoja na dira za maendeleo ya Taifa ya mwaka 2030 hivyo wananchi wanatakiwa kumuunga mkono kwa kuhakikisha anapata ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu ujao.

Pamoja hayo alitoa wito kwa wananchi wote wanaoamini,kupenda na kuridhishwa na sera za leo Chama Cha Mapinduzi wajitokeze kujiunga na Chama hicho ikiwa ni sehemu ya kudumisha demokrasia na maendeleo endelevu kwa wote.

Alisema CCM itaendelea kufanya siasa za kistaarabu kwa kuheshimu sheria na miongozo ya nchi na kwamba Chama Kuna dhima ya kulinda amani na utulivu wa nchi.

No comments: