Thursday, September 12, 2024

NBAA YAHITIMISHA MAFUNZO


Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania ( NBAA) CPA Pius A. Maneno akizungumza wakati wa kufunga mafunzo kwa Wakufunzi kutoka Vyuo mbalimbali wanaosaidia Shughuli mbalimbali za Bodi iliyofanyika katika Ofisi za NBAA jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Elimu ya Taaluma na Mafunzo NBAA, Peter Lyimo (kulia) akitoa maelezo kuhusu namna semina hiyo ilivyendeshwa kwa Wakufunzi kutoka Vyuo mbalimbali  wanaofanya shughuli mbalimbali za Bodi.

BODI ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imehitimisha mafunzo kwa wataalam kutoka vyuo na taasisi wanaofanya shughuli mbalimbali za Bodi ili kuhakikisha viwango vipya vya mabadiliko ya mtaala vinafuatwa.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo ya siku mbili Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania ( NBAA) CPA Pius A. Maneno amesema teknolojia imebadilika hivyo na wao sasa ni wakati umefika wanatakiwa kubadilika na pia wataalamu wanapaswa kuwa mabalozi wa mabadiliko akisisitiza kuwa mitihani inapaswa kupima ujuzi halisi na sio kutumia teknolojia kama akili bandia (AI) inayoweza kutoa majibu ya nadharia, ambayo hayapimi uwezo wa mwanafunzi.

Ametoa shukrani kwa wakufunzi na washiriki wa mafunzo hayo yaliyolenga kuleta mabadiliko hasa kwa kipindi hiki cha Mtaala mpya na kuongeza kuwa elimu waliyoipata itawasaidia pia kwenda kuitumia huko vyuoni.

Maneno aliwapongeza washiriki kwa kujitolea kujifunza mbinu mpya na teknolojia zinazohusiana na utungaji wa mitihani na umuhimu wa wataalamu wa uhasibu kutumia maarifa waliyoyapata kusaidia wengine na kuboresha sekta nzima ya uhasibu nchini.

Naye mmoja wa washiriki alisema mafunzo hayo yanalenga hasa ni kwanini wanafunzi wanafeli hivyo wanaelekezwa namna nzuri ya kutunga mitihani kwa kuangalia mtaala unavyoelekeza ili kuepuka kutoka nje ya mtaala na kuweza kumpima mtahiniwa wa Bodi uelewa wake katika hatua aliyopo.

Pia mafunzo hayo yamewapa uelewa zaidi kuhusu usimamizi wa mitihani na mbinu bora za kujenga wanafunzi wenye uwezo wa kuhimili changamoto za soko la ajira kwa weledi wa kutosha. 

No comments: