Tuesday, October 1, 2024

BALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI NA MGENI WAKE WAZIRI WA OFISI YA RAIS MIPANGO NA UWEKEZAJI WAKIWA WAGENI WA HESHIMA MTANANGE WA SIMBA NA YANGA AUSTIN, TEXAS.

Mtanange wa Simba na Yanga Austin, Texas umeisha kwa Yanga kufungwa kwa taaabu na Simba. Kipindi cha kwanza Simba ilitangulia kwa kupata mabao mawili ya haraka yaliyofungwa na James Kittilya dakika ya 2 tu ya mchezo na la pili lilifungwa na Micky JR dk ya 35 ya mchezo. Yanga walichangamka dakika ya 36 na kupata bao la penalty kupitia kwa nyota wao kijana Ally Ngolo na dakika chache kabla ya mapumziko walipata bao la kusawazisha kupitia kwa mshambiliaji wao Richard Mbappe ingawa mfungaji alikuwa ameotea lakini refa Ricky Reynolds maarufu kama Bongozozo Timu ya Yanga walimtilia mashaka refa Bongozozo baada kujisahau na kushangilia goli alilofunga mwanae Micky. Ukiondoa kasoro hii refa aliweza kubalansi mchezo.

 Kipindi cha pili Simba waliingia kwa nguvu na kupata mabao matatu ya haraka yaliyofungwa na Kelvin Onesmo dk 48, Kisuby Warro dk ya 64 na Justice Munissi dakika ya 72 kabla yanga hawajapata bao la tatu kupitia kwa Ally Ngolo tena dk ya 86. Hadi muamuzi anapuliza filimbi ya mwisho Simba 5-3 Yanga. Mgeni rasmi alikabidhi kombe la DICOTA CONVENTION CUP kwa msimu wa 2024-2025 kwa kocha/mchezaji wa Simba Maestro Cassius Pambamaji na kuanzisha shangwe na nderemo kutoka kwa mashabiki wa timu zote mbili. *video ni Simba wakikabidhiwa kombe lao na wachezaji na mashabiki wakishangilia* Tukutane msimu ujayo Yanga wajipange vizuri
Mhe. Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Dkt. Elsie Kanza akiwa na mgeni wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, wakiwasili uwanjani kushuhudia mtanange wa watani wa jadi, Simba vs Yanga mechi iliyofanyika siku ya Jumampso Septemba 28, 2024 Austin, Texas na  Simba kuibuka na ushindi wa 5G zidi ya Yanga.Picha na Vijimambo Blog.
Wawakilishi wa CRDB Mercy Nkini (wapili toka kulia na Wilson Mzava (kulia) ambao walidhamini jezi na kombe kwenye mechi hiyo ya Simba na Yanga
Kepteni wa Yanga Eddie akikabidhiwa jezi ya Yanga na mdhamini CRDB Mercy Nkini 
Kepteni wa Simba Cassihno akikabidhiwa jezi ya Simba na mdhamini CRDB Mercy Nkini
Mhe. Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Dkt. Elsie Kanza akisalimiana na Haji Manara  semaji la Yanga Marekani kabla ya mechi wakati wa Mhe. Balozi na mgeni wake walipokua wakisalimiana na wachezaji.
Mhe. Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Dkt. Elsie Kanza akiwa na mgeni wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo wakiongea jambo na Bongo Zozo kabla ya zoezi la ukaguzi wa timu mbili.
Mhe. Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Dkt. Elsie Kanza akiwa na mgeni wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo wakiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Simba,
Mhe. Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Dkt. Elsie Kanza akiwa na mgeni wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo wakiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Yanga.
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi

No comments: