ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, October 31, 2024

RAIS MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN ASHIRIKI MJADALA KUHUSU KILIMO BARANI AFRIKA ULIOFANYIKA, DES MOINES, IOWA NCHINI MAREKANI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki kwenye mjadala (round tables discussion) kuhusu Kilimo barani Afrika, katika Mji wa Des Moines, Iowa nchini Marekani tarehe 30 Oktoba, 2024. Mjadala huo ambao uliandaliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka barani Afrika, Serikali na Sekta binafsi ya Marekani hususan waliopo kwenye sekta ya kilimo.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza kwenye mjadala (round tables discussion) kuhusu Kilimo Barani Afrika pamoja na Nishati Safi ya Kupikia katika Mji wa Des Moines, Iowa nchini Marekani tarehe 30 Oktoba, 2024. Kushoto ni Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina akimsikiliza. Rais Dkt. Samia alishiriki mjadala huo kando ya mjadala wa Kimataifa wa Norman E. Borlaung ambao umeandaliwa na Taasisi ya World Food Foundation








Viongozi mbalimbali wakifuatilia mjadala kuhusu Kilimo Barani Afrika katika Mji wa Des Moines, Iowa nchini Marekani kando ya mjadala wa Kimataifa wa Norman E. Borlaung ambao umeandaliwa na Taasisi ya World Food Foundation tarehe 30 Oktoba, 2024.

No comments: