Wednesday, November 6, 2024

DKT. MWAMBA ATETA NA UJUMBE KUTOKA EU


Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akiagana na Mkuu wa Masuala ya Ushirikiano wa Umoja wa Ulaya nchini, Bw. Marc Stalmans, alieongoza Timu ya Wataalamu kutoka Umoja wa Ulaya baada ya kikao chao kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Katibu Mkuu, jijini Dodoma, ambapo walijadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Serikali na Umoja wa Ulaya na tathmini ya programu ya Neighbourhood Development International Cooperation Instrument (NDICI) na Multi-annual Indicative Programme 2021-2027 (MIP 2021-2027) kwa kipindi cha miaka minne ya utekelezaji, 2021-2024.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akizungumza wakati wa kikao chake na Timu ya Wataalamu kutoka Umoja wa Ulaya nchini Tanzania ikiongozwa na Mkuu wa Masuala ya Ushirikiano wa Umoja wa Ulaya nchini, Bw. Marc Stalmans (hayupo pichani), katika ukumbi wa Mikutano wa Katibu Mkuu, jijini Dodoma, ambapo walijadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Serikali na Umoja wa Ulaya, na tathmini ya programu ya Neighbourhood Development International Cooperation Instrument (NDICI) na Multi-annual Indicative Programme 2021-2027 (MIP 2021-2027) kwa kipindi cha miaka minne ya utekelezaji, 2021-2024.
Kikao cha Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Timu ya Wataalamu kutoka Umoja wa Ulaya nchini iliyoongozwa na Mkuu wa Masuala ya Ushirikiano wa Umoja wa Ulaya nchini, Bw. Marc Stalmans, kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Katibu Mkuu, jijini Dodoma, ambacho kilijadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Serikali na Umoja wa Ulaya na tathmini ya programu ya Neighbourhood Development International Cooperation Instrument (NDICI) na Multi-annual Indicative Programme 2021-2027 (MIP 2021-2027) kwa kipindi cha miaka minne ya utekelezaji, 2021-2024.
Mkuu wa Masuala ya Ushirikiano wa Umoja wa Ulaya nchini, Bw. Marc Stalmans, aliyeongoza Timu ya Wataalamu kutoka Umoja wa Ulaya nchini, akizungumza jambo wakati wa kikao chao na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (hayupo pichani), kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Katibu Mkuu, jijini Dodoma, ambapo walijadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Serikali na Umoja wa Ulaya na tathmini ya programu ya Neighbourhood Development International Cooperation Instrument (NDICI) na Multi-annual Indicative Programme 2021-2027 (MIP 2021-2027) kwa kipindi cha miaka minne ya utekelezaji, 2021-2024.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (wa tano kushoto), Mkuu wa Masuala ya Ushirikiano wa Umoja wa Ulaya nchini, Bw. Marc Stalmans, aliyeongoza Timu ya Wataalamu kutoka Umoja wa Ulaya, wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa waandamizi wa Wizara ya Fedha na Wataalamu kutoka Umoja wa Ulaya nchini, baada ya kikao chao kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Katibu Mkuu, jijini Dodoma, ambacho kilijadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Serikali na Umoja wa Ulaya na tathmini ya programu ya Neighbourhood Development International Cooperation Instrument (NDICI) na Multi-annual Indicative Programme 2021-2027 (MIP 2021-2027) kwa kipindi cha miaka minne ya utekelezaji, 2021-2024. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)

Na. Joseph Mahumi na Chedaiwe Msuya, WF, Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na Timu ya Wataalamu kutoka Shirika la Umoja wa Ulaya iliyoongozwa na Mkuu wa Ushirikiano wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Bw. Marc Stalmans, katika ukumbi wa Mikutano wa Katibu Mkuu, jijini Dodoma.

Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni tathmini ya utekelezaji wa maeneo ya vipaumbele vya ushirikiano vilivyokubalika katika kipindi cha Miaka 7 kuanzia mwaka 2021 hadi 2027, Mpango wa kijani (Green Deal), Mtaji wa Watu na Ajira (Human Capital and Employment) na Utawala (Governance)) maarufu kama Multiannual Indicative Programme 2021-2027.

Aidha walikubaliana juu ya mwelekeo wa uandaaji wa miradi mipya kwa mwaka 2025 (Annual Action Plan 2025 - AAP 2025).

Pamoja na Mambo mengine walitoa taarifa fupi ya utekelezaji wa awamu ya kwanza kwa miaka minne (4) ambao umetekelezwa kwa mafanikio makubwa, ambapo jumla ya EURO 366 Millioni (sawa na trilioni 1.075 za kitanzania) zimetengwa kwenye miradi 6 ya kitaifa na EURO 141 Milioni (sawa bilioni 414.17 za kitanzania) zimetengwa kwenye miradi ya kikanda inayoendelea.

Hadi sasa Umoja wa Ulaya umeidhinidha utekelezaji wa awamu ya pili wa mpango huo ambapo kiasi cha EURO 219 Millioni (sawa bilioni 641.95 za kitanzania) zitaelekezwa kwenye vipaumbele vya awali pamoja na Miradi inayohusu Malighafi Muhimu (Critical Raw Materials).

Kikao hicho kilihudhuriwa na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. James Msina, Mkuu wa Masuala ya Msaada kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya, Kitengo cha Uratibu na Ushirikiano, Bw. Jonathan Mpuya, Mkuu wa Fedha na Utawala - Kitengo cha Uratibu na Ushirikiano, Bw. Ibrahim Muhazi, Afisa wa Mpango wa Rasilimali Asili, Bw. Leonard Lema, na maafisa wengine kutoka Umoja wa Ulaya nchini.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake