Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe limefanya uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Shule ya Sekondari ya Sumagha iliyopo Mjini Tunduma Wilaya ya Momba Mkoani Songwe.
Uzinduzi huo umefanywa na Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya ya Momba Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Bahati Simchile Novemba 26, 2024 akiwa shuleni hapo alitumia wasaa huo kutoa elimu kwa wanafunzi juu ya madhara ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto.
Aidha, Mkaguzi Simchile amewaeleza wanafunzi suala la umuhimu wa kutoa taarifa za ukatili kwa Jeshi la Polisi ili kukabiliana na matukio hayo ambayo yanaiathiri jamii katika ustawi wa familia moja moja na Taifa kwa ujumla.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe limekusudia kutoa elimu ya kubaini na kuzuia matukio hayo kwenye maeneo na makundi mbalimbali ikiwemo mashuleni, Nyumba za Ibada, Sokoni, Stendi, Vijiwe vya Bodaboda na maeneo yenye mkusanyiko wa watu wengi ili kutokomeza vitendo hivyo ndani ya Mkoa wa Songwe na viunga vyake.
Ikumbukwe kuwa kila ifikapo Novemba 25 hadi Disemba 10 kila mwaka Tanzania uungana na mataifa mengine duniani kupinga ukatili wa kijinsia kwa siku 16 ikiwa ni kuonyesha msisitizo kwenye jambo hilo ili jamii iweze kuchukia na kuacha kutenda vitendo hivyo ili jamii iendelee kuwa salama.

No comments:
Post a Comment