Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA Leonard Mkude akisoma hotuba ya ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka 2024 wa wahasibu na wakaguzi wa hesabu ulioandaliwa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) uliofanyika katika hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam. Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA Leonard Mkude alimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA. Prof. Sylvia S. Temu akizungumza kuhusu mikakati mbalimbali ya kusimamia Taaluma ya Uhasibu na Ukaguzi wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka 2024.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania(NBAA), CPA Pius A. Maneno akisoma risala kwa mgeni rasmi kusuhu namna wanavyosimamia wahasibu pamoja na wakaguzi wanapokuwa kazini ili kulinda taaluma zao wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka 2024 uliofanyika leo Novemba 28, 2024 katika hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA Leonard Mkude(kushoto) akimkabidhi cheti cha heshima Mwenyekiti Mstaafu wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Simon Fundi Sayore wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka 2024.
Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA Leonard Mkude(kushoto) akimkabidhi cheti cha heshima CPA Simon Mponji wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka 2024.
Baadhi ya wa wahasibu na wakaguzi wa Hesabu wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA Leonard Mkude aliyemwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka 2024 wa Wahasibu na Wakaguzi wa hesabu uliofanyika katika hoteli ya APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Picha za pamoja
MHASIBU Mkuu wa Serikali, CPA Leonard Mkude, amewataka wahasibu kuzingatia maelekezo ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) kuhusu namna ya kuripoti masuala ya mabadiliko ya Tabianchi na kutumia fursa zilizopo ili kuboresha uzalishaji wa kiuchumi na kuchangia katika maendeleo endelevu nchini.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika Mkutano mkuu wa mwaka 2024 wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Leonard Mkude ameeleza kuwa Wahasibu wana nafasi muhimu katika mnyororo wa uzalishaji wa kiuchumi hasa katika kukabiliana na mabadiliko ya teknolojia kama vile matumizi ya akili bandia katika ukuaji wa uchumi.
“Wahasibu ni kiungo muhimu katika mipango na matumizi ya fedha, hasa katika juhudi za Tanzania kufikia uzalishaji wa hewa chafu sifuri ndani ya miaka 50,” amesema CPA Mkude.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA, Prof. CPA Sylvia Temu amesema Mkutano huo wa siku tatu una malengo mawili makuu, likiwemo kubadilishana maarifa na uzoefu wa kitaaluma ili kubaini fursa na changamoto zinazokabili tasnia ya Uhasibu.
“Pia tumejadili uelekeo wa nchi kwa miaka 25 ijayo, ambapo Wahasibu wanapaswa kushiriki kikamilifu kubaini fursa za kuendeleza uchumi wa taifa letu na kuleta mchango wenye thamani katika maendeleo ya nchi,” amesema Prof. Temu
Mwanachama wa heshima wa NBAA, CPA Saimon Sayore amewataka vijana kuipenda taaluma ya Uhasibu, kuitumikia kwa uaminifu na kuhakikisha wanatunza vyema fedha za Taasisi na taifa kwa ujumla.
Mkutano huo unajumuisha mawasilisho na majadiliano mbalimbali yanayolenga kutoa suluhisho kuhusu mchango wa Wahasibu katika kukabiliana na mabadiliko ya kiteknolojia na kuimarisha Maendeleo endelevu.
No comments:
Post a Comment