ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, November 26, 2024

YOHANA LUHEMEJA AFUNGA KAMPENI ZA UENYEKITI WA SERIKALI ZA MITAA KWA KISHINDO MTAA WA MBWAMAJI

 


Na. Andrew Chale, Kigamboni.


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mtaa wa Mbwamaji kimefunga kampeni zake kwa kishindo za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambapo Wananchi watapiga kura siku ya Kesho Jumatano Novemba 27, mwaka huu nchini kote.


Kampeni hizo  Mgombea Uenyekiti kwa CCM Yohana Luhemeja, aliyeongozana na wagombea nafasi ya Ujumbe akiwemo Masenga Kiwango, Zubeir Fuko,  Christopher Mabwai, Naim Pazi na Fatma Sima ambao kwa pamoja wameomba kura kwa Wana Mbwamaji ilikufanikisha maendeleo ngazi ya Serikali ya Mtaa huo.


Awali akinadi sera zake Mgombea Uenyekiti Yohana Luhemeja amesema kipaombele ni kujenga shule ya Msingi, Zahanati, barabara pamoja na kuchimba Visima viwili Kanda ya Maduka mawili ilikufikisha maji eneo hilo sambamba na kumalizia upimaji wa ardhi mtaa wa mbwamaji.



"Niwaombeni Wana Mbwamaji, nina uzoefu wa mtaa huu. Kura yenu Novemba 27, ni muhimu na itaniwezesha kusimamia Afya, Miundombinu, Elimu na Mazingira lakini pia kusimamia upatikanaji wa mikopo kwa makundi maalum ya Vijana na Wanawake". Amesema Yohana katika kampeni hiyo.


Nilikuwa na utaratibu wa kuitisha mikutano ya Wananchi kila baada ya miezi mitatu (3) na hii ilisaidia sana maendeleo ya Mbwamaji, naombeni kura zenu Novemba 27 kuendeleza hili" Amesema Yohana Luhemeja.










No comments: