Na John Walter -Mbulu
Hakimu mkazi wa Mahakama ya Mwanzo Dongobesh, Mgusi Clifford Masinde, amewataka Wenyeviti wa vijiji, Wenyeviti wa vitongoji, Wajumbe mchanganyiko na Wajumbe kundi la wanawake kufanya kazi kwa utii na uadilifu katika maeneo yao.
Hayo ameyasema wakati akiwaapisha viongozi wa Serikali za mitaa wateule, katika kata ya Tumati, Yaeda ampa, Masqaroda, Masieda, Endahagichan, Yaeda chini, Eshkesh na Bashay, Novemba 29, 2024.
Mgusi amesema viongozi hao wanaenda kuitumikia jamii, hivyo wafanye kazi katika misingi ya kisheria iliyonyooka kwa utii na uadilifu kwa mujibu wa viapo walivyopata huku wakifanya kazi kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zote illi kuweza kutimiza malengo ya serikali.
Aidha kwa upande wa Kiongozi wa dini Askofu mstaafu wa KKKT Dayosisi ya Mbulu, Zebedayo Daudi, ameipongeza Serikali kwa kusimamia uchaguzi vyema na kumalizika salama bila kuwa na vurugu.
"Siasa ni ushindani, asiyekubali kushindwa sio mshindani na uongozi ni kupeana kijiti kwa faida ya nchi yetu, na sasa hivi kama chaguzi zimeisha tuelekee kwenye kazi zetu za kila siku" alisema askofu Zebedayo.
No comments:
Post a Comment