ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 9, 2026

SIMBA WANYIKA NA ASILI YAO

 

Pichani ni kundi la vijana wa jamhuri jazz

Makundi yote ya Wanyika yalikuwa yamejikita nchini Kenya, ingawa viongozi wake wakuu, ndugu wa Kinyonga (Wilson na George), Omar Shabani, John Ngereza na Issa Juma wote walitokea Tanzania na walijifunza na kukomaa kimuziki katika mazingira yenye rutuba ya muziki wa Tanzania wa miaka ya 1960 na 1970.

Orodha hii ya kazi za muziki (discography) iliwekwa mtandaoni kwa mara ya kwanza tarehe 10 Julai 2004. 

Taarifa nyingi za awali zilitolewa na Doug Paterson, ambaye ukurasa wake wa East African Music Page ni moja ya vyanzo muhimu vya habari kuhusu muziki wa Kenya na Tanzania.

Baadaye mwandishi aliwasiliana na Peter Toll kutoka Uholanzi, ambaye alidhamini ziara mbalimbali za Simba Wanyika mwishoni mwa miaka ya 1980 na mwanzoni mwa miaka ya 1990. 

Peter Toll aliandika makala mbili muhimu kuhusu Wanyika, The Wanyika Weave (1991) na Wanyika Memories (1993), na pia alikuwa mtayarishaji wa CD ya Simba Wanyika Pepea mwaka 1992.

Peter Toll alitoa taarifa nyingi kuhusu rekodi ambazo hazikuwepo katika orodha ya awali. 

Aidha, makala zake zilitoa maelezo muhimu ya ziada na marekebisho ya taarifa zilizokuwepo.

Kwa msaada wa taarifa zaidi kutoka Doug Paterson na Michael Kieffer, toleo hili jipya la "Discography of the Wanyika Groups" limekuwa zaidi ya mara mbili ya ukubwa wa toleo la kwanza.


John Beadle


JAMHURI JAZZ BAND

Jamhuri Jazz ilianzishwa Tanga, Tanganyika mwishoni mwa miaka ya 1950 na ilikuwa moja ya bendi maarufu zaidi Tanzania.

Wilson Peter Kinyonga na George Peter Kinyonga waliingia katika bendi hiyo mwaka 1966 na walipiga humo kwa miaka minne kabla ya kuondoka Desemba 1970 kuanzisha Arusha Jazz Band.

Maelezo yaliyopo kwenye albamu Simba Wanyika Greatest Hits Vol. 1 yanadai kuwa baada ya wao kuondoka bendi ilisambaratika, lakini jambo hilo si kweli. 

Jamhuri Jazz iliendelea kupiga muziki hadi angalau miaka ya 1970.

Katika kipindi hicho, baadhi ya wanachama wake akiwemo Omar Shabani walichukuliwa na ndugu wa Kinyonga kujiunga na Simba Wanyika.

Baadhi ya nyimbo zake zilikuwa:

Mpenzi Fikiri

Dunia Imenisonga

Bibi Mwenye Chongo

Simba Mwituni

Shingo ya Upanga

Nafikiria Kurudi Shamba

Susana

Magdalena


ARUSHA JAZZ BAND

Arusha Jazz ilianzishwa Arusha mwaka 1971 na Wilson Kinyonga, George Kinyonga, ndugu yao William Kinyonga pamoja na wanamuziki wengine watatu.


Kwa mujibu wa maelezo ya albamu Simba Wanyika Greatest Hits Vol. 1, nyimbo kadhaa ambazo baadaye zilijulikana kama za Simba Wanyika kama:

Pamela

Kenya Yetu

Marceline

zilirekodiwa kwanza chini ya jina la Arusha Jazz.

Mwezi Juni 1971 bendi ilihamia Mombasa, Kenya na kubadili jina kuwa Simba Wanyika (Simba wa Porini).

Hata hivyo jina la Arusha Jazz halikufa mara moja. Peter Toll anaeleza kuwa walipofika Mombasa walikuwa na mabango mawili jukwaani:

Simba Wanyika

Arusha Jazz

George Kinyonga alisema walitumia majina yote mawili kwa muda, lakini kuanzia mwaka 1973 walibaki kutumia jina la Simba Wanyika pekee.

Nyimbo zao za mwanzo zilikuwa:

Mama Suzie

Mary Mtoto

Tutengane Salama

Mama Niache

Eliza Wangu

Jose Twende Zaire

Mwaka 1987 kulitolewa kaseti ya mkusanyiko wa nyimbo zao za zamani iliyoitwa Mama Suzie.

ORCHESTRA SIMBA WANYIKA

Ingawa Simba Wanyika ilikuwa mwendelezo wa Arusha Jazz, kati ya mwaka 1971 na 1973 kulikuwa na mabadiliko mengi ya wanachama.

Peter Toll anaandika kuwa kufikia mwaka 1973 wapiga muziki wa awali walikuwa wamebadilika na:

Rashid Juma (mpiga ngoma kutoka Tanga)

Tom Malanga (mpiga bass kutoka Mombasa)

Katika safari nyingine ya Tanzania, ndugu wa Kinyonga waliwachukua wanamuziki wawili kutoka Jamhuri Jazz:

Elias John (saxophone)

Omar Shabani (rhythm guitar), ambaye baadaye alijulikana kama Professor Omar

Katika kipindi hicho bendi ilisaini mkataba na Polygram Kenya.

Baada ya miaka minne Mombasa, Simba Wanyika ilihamia Nairobi na kwa zaidi ya miaka ishirini ikawa moja ya bendi muhimu zaidi katika maendeleo ya muziki wa Afrika Mashariki.

Mtindo wa Muziki wa Simba Wanyika

Doug Paterson anaeleza kuwa kama bendi nyingi za Tanzania, Simba Wanyika walicheza rumba yenye mashairi ya Kiswahili.

Tofauti na mtindo wa Benga uliokuwa unaibuka Kenya wakati huo, muziki wao ulikuwa:

laini zaidi, mtulivu, unaotiririka

Rekodi zao za mwanzo hazikuwa hata na drum set.

Mdundo ulitokana na:

Congas na Claves na midundo ya Cavacha kwenye hi-hat

Gitaa la rhythm lilikuwa linafanya kazi nyingi lakini kwa sauti ya upole, huku solo guitar na saxophone zikitumika kwa vipindi maalumu tu.

Peter Toll anaeleza kuwa sauti za Wilson na George zilipoimbwa kwa pamoja ziliunda alama maalumu ya Simba Wanyika ambayo iliwavutia mashabiki wengi sana.

MGOGORO NA KUANZISHWA KWA LES WANYIKA

Kama ilivyo kwa makundi mengi ya muziki Afrika, mafanikio yalileta migogoro.


Mwaka 1978 wanachama kadhaa wa Simba Wanyika wakiongozwa na Omar Shabani waliondoka na kuunda Les Wanyika.

Mwaka 1980 mgogoro mwingine kati ya George na Wilson Kinyonga ulisababisha kuundwa kwa Orchestra Jobiso. Hata hivyo mgogoro huo ulimalizika baadaye.

KUREJEA KWA NGUVU KWA SIMBA WANYIKA

Baada ya changamoto hizo, Simba Wanyika ilijikusanya upya. Mwaka 1983 walitoa kibao kikubwa sana:

Shilingi

Kibao hicho kilifuatwa na nyimbo nyingine zilizofanikiwa sana kama:

Halleluya

Baba Asiya


Peter Toll anaeleza kuwa Shilingi iliuza karibu nakala 50,000 wakati ambapo biashara ya muziki ilikuwa tayari imeanza kuathiriwa na uharamia wa kazi za sanaa.


KUONDOKA KWA WANAMUZIKI MUHIMU


Mwaka 1976 wanamuziki hawa waliondoka Simba Wanyika na kurudi Tanzania:

Luiza Elias John (tenor saxophone)

Kassim Mponda Mbwana (mi-solo guitar)

Bindo Bakari Kipanga (rhythm guitar)


Sababu kubwa ilikuwa kusambaratika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ya wakati huo.


Luiza Elias John baadaye alijiunga na Mwenge Jazz ya JWTZ.

Mwandishi Miguel Suleyman aliwahi kusema:  "Luiza Elias alikuwa mwanamuziki aliyesoma zaidi katika historia yote ya Wanyika. 

Linganisha muziki wa Simba Wanyika kabla na baada ya kuondoka kwake."

WIMBO WA NAKUPENDA

Mwaka 1977 Simba Wanyika walitoa wimbo:

Nakupenda

Ingawa uliandikwa na George Kinyonga, haukuwa toleo la awali la Nakupenda Sherry ambayo baadaye ilikuja kuwa hit kubwa ya Orchestra Jobiso.

Peter Toll alisema:

"Huu ulikuwa wimbo wenye nguvu sana uliochezwa katika mdundo wa Moja Moja." Moja moja na simba wa nyika


SIKUJUA UTABADILIKA


Baada ya wanachama wengi kuondoka mwaka 1978 kuunda Les Wanyika, Wilson na George waliunda kikosi kipya chenye:

Joseph Tito (rhythm guitar)

George Madrago (bass)

Maneno Shaban Ally (drums)

Kwa kikosi hicho walirekodi:

Sikujua Utabadilika kama kuthibitisha kuwa Simba Wanyika bado ilikuwa bendi imara licha ya mabadiliko ya wanachama.


ZIARA YA ULAYA

Mwaka 1989 Simba Wanyika ilipojiandaa kwa ziara yake ya kwanza Ulaya ilikumbwa na tatizo kubwa.


Ni Wilson na George Kinyonga pekee waliokuwa na pasipoti.

Kwa hiyo walilazimika kuchukua wanamuziki watatu kutoka bendi ya Africa Jambo Jambo:


Sammy Kasule (Uganda)

Coco Kanyinda (DR Congo)

Micky Jaga Jaga (DR Congo)


Peter Toll anasema kwamba ingawa kikosi hicho hakikuwa Simba Wanyika ya kawaida, kilipiga nyimbo za Kinyonga kwa ustadi mkubwa na kupokelewa vizuri sana Ulaya.


ALBAMU YA PEPEA

Mwaka 1992 Simba Wanyika ilitoa CD ya: Pepea


iliyorekodiwa nchini Uholanzi wakati wa ziara yao ya dunia ya mwaka 1991.


Nyimbo zake zilijumuisha:

Mwongele, Wenzako, Pamela

Sikujua Utabadilika, Nakupenda Cherie, Pole Pole, Maria


Mbali na Wilson na George Kinyonga, wanamuziki wengine walikuwa:

Maneno Shaban Ally

Mike Beche

Victor Boniface


KIFO CHA GEORGE NA WILSON

George Peter Kinyonga alifariki mkesha wa Krismasi mwaka 1992 baada ya kuugua kwa muda mfupi.


Wilson Peter Kinyonga naye alifariki mwaka 1995.


Baada ya vifo vya ndugu hao wawili, Simba Wanyika ilianza kufifia na hatimaye kuvunjika.


Peter Toll alieleza kuwa kaseti moja iliyotolewa baadaye kwa jina la Simba Wanyika haikuwa ya bendi halisi, bali ya mtu kutoka Tanzania aliyedai kuwa ni ndugu wa familia ya Kinyonga na alitaka kuendeleza jina la Simba Wanyika. Hata hivyo hakusikika tena baada ya kutuma kaseti hiyo.


(Sehemu zinazofuata za Les Wanyika, Les Moto Moto, Orchestra Jobiso, Super Wanyika Stars, Everest Kings na Great Sounds 


Itaendelea........


Makala haya kwa hisani ya : BARIKI NGOWO -MUZIKI HALISI 

No comments: