Na. Elisa Niarira Mrutu
0787356060
Mtoto wa "Dwarf, Kutoka Rosario
Lionel Andrés Messi alizaliwa 24 Juni 1987 huko Rosario, Argentina. Alikuwa mtoto wa 3 kati ya 4. Familia ya kawaida tu baba yake alifanya kazi kiwandani, mama yake alifua nguo.
Umri wa miaka 11 daktari akagundua ana ugonjwa: Growth Hormone Deficiency [GHD]. Maana yake mwili wake haukutoa homoni ya kukua. Kama hangepewa sindano kila siku, asingekuwa mkubwa zaidi ya futi 4'3. Gharama ya sindano ilikuwa dola $900 kwa mwezi. Familia yake haikuwa na hizo pesa.
Vilabu vya Argentina vikasema ,Tunapenda kipaji chake, lakini hatuwezi kulipia matibabu yake. Ndoto yake ya kuwa mchezaji ilikuwa inaisha kabla hata haijaanza.
Safari ya Barcelona na Sindano 1000
Akiwa na miaka 13, msimamizi wa talenti wa Barcelona alimwona akicheza kwao Argentina. Barcelona wakasema tutakuchukua, tutakulipia matibabu yako yote, Shida? Messi alikuwa Argentina, Barcelona Uhispania.
Baba yake Jorge akaacha kila kitu. Akamchukua Messi na ndugu zake, wakapanda ndege kwenda Spain bila kujua Kihispania vizuri. Messi kila siku kwa miaka 3 alichomwa sindano mguuni. Alilia, aliogopa, lakini hakuwahi kukosa Alisema, "Nilichagua kuumia kwa sindano ili nisiume kwa majuto maisha yangu yote".
Alipona. Urefu wake ukafika futi 5'7". Leo hii bado ni mfupi kama mchezaji, lakini ndio "urefu kamili" wa dribbling yake.
Alifanya Nini Kwenye Maisha Yake - Mafanikio
Klabu Barcelona 2004-2021,
Alivunja rekodi zote. Magoli 672 kwa Barcelona rekodi ya mchezaji 1 klabu 1 duniani. Akatwaa Ballon d'Or mara 8 - mtu pekee kuwahi kufika hapo. Akawaongoza Barcelona kuchukua Champions League mara 4.
Staili yake ni tofauti, hajisumbui kukimbia sana, lakini mpira ukiwa miguuni mwake unashikamana kama gundi. Watu humwita "Mchawi mdogo".
Timu ya Taifa Argentina
Hapa ndio watu walimkosoa sana. Miaka 16 alicheza finali 4 na kupoteza zote. Watu wa Argentina wakasema ,Haipendi nchi yake kama Maradona, Mwaka 2016 hata alistaafu kwa hasira baada ya kupoteza fainali ya Copa America.
Lakini akarejea. Mwaka 2021 alitwaa Copa America - kombe lake la kwanza na Argentina. 2022 akatimiza ndoto, Akatwaa Kombe la Dunia Qatar 2022, Alifunga magoli 7, akawa mchezaji bora wa mashindano yote. Watu wote wakakubali,Sasa Messi ni GOAT kamili.
Nje ya Uwanja
1. Mfadhili ana foundation yake ,Leo Messi Foundation inayosaidia watoto 200,000+ kupata elimu na matibabu duniani kote. Yeye mwenyewe alikuwa mtoto mgonjwa, hivyo anajua maumivu ya wazazi.
2.Mnyenyekevu, Hapendi kelele, hapendi maneno mengi. Baada ya kushinda Kombe la Dunia, alisema tu: "Nilikuwa nina deni kwa nchi yangu, Leo nimelipa.
3. Mwaminifu, Ameoa mpenzi wake wa utotoni Antonella. Hana skendo, hana matatizo. Alisema ,Familia yangu ndio tuzo yangu kubwa kuliko Ballon d'Or na alimweka baba yake kuwa meneja wake kwa kutambua mchango wa baba yake.
MAFUNZO MAKUBWA 4 KUBWA KUTOKA MAISHA YA MESSI
1. Udogo sio kikwazo Watu walimwambia we ni mfupi, huwezi. Leo ni mfupi zaidi kuwahi kushinda Ballon d'Or. Akatumia udogo wake kama silaha ni mgumu kumshika kwa sababu kituo chake cha mvuto ni chini, na hakutishwa na kelele za watu.
2. Baada ya maumivu huja furaha,
Sindano 1000 kwa miaka 3. Hakuna talenti bila maumivu. Talenti na nidhamu zimempa historia.
3. Usiache wakati watu wanacheka, Argentina ilimcheka kwa 16 miaka. 2022 akawanyamazisha wote. Kombe la Dunia ndio jibu lake.
4. Mshinde kimya, Messi hana kelele Anafanya kazi, anafunga, anarudi nyumbani kwa familia. Alionyesha unaweza kuwa bora bila kupiga kelele.
Nukuu yake maarufu ya Messi.
"Utalazimika kujitahidi mara 10 zaidi ya wengine kama unataka kufanikiwa. Nilifanya hivyo nikawa mdogo, na bado nafanya hivyo leo".




No comments:
Post a Comment