ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 2, 2026

TANAPA YANG’ARA KIMATAIFA YATUNUKIWA TUZO YA UBORA 2026 UBELGIJI

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Nkoba Mabula


Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limeendelea kuipeperusha bendera ya Tanzania kimataifa. Hii ni baada ya kutunukiwa Tuzo ya Mafanikio katika Ubora ya mwaka 2026 (Quality Achievement Award 2026) tarehe 31 Mei 2026 jijini Brussels, Ubelgiji, inayotolewa na Taasisi ya _European Society for Quality Research_ (ESQR)

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Nkoba Mabula, ameipongeza TANAPA kwa kuendelea kutoa huduma zenye kukidhi  ubora wa viwango vya kimataifa.

Kwa upande wake, Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA, CPA (T) Musa N.K.Juma amesema TANAPA imepokea tuzo hiyo kwa mara ya nane mfululizo, na kwamba huu ni uthibitisho wa ubora wa huduma za TANAPA na jitihada za kimkakati za kuitangaza Tanzania kama kitovu cha utalii duniani.

Kamishna wa Uhifadhi CPA (T) Kuji, ameongeza kuwa mafanikio hayo yanaakisi jitihada za Serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuimarisha sekta ya utalii na kuitangaza Tanzania katika masoko ya kimataifa.



#ESQR2026 #MNRT #DestinationTanzania #TANAPA #TanzaniaUnforgettable #QualityAchievementAwards

No comments: