Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeendelea kusisitiza umuhimu wa watumishi wake kuzingatia muda na maadili ya kazi ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za afya kwa wananchi.
Akitoa mada wakati wa Kikao cha 31 cha Baraza la Wafanyakazi wa MNH, Balozi Omary Kashera NDC, amesema matumizi sahihi ya muda ni muhimu katika kupunguza changamoto za kiutendaji na kuongeza tija mahali pa kazi. Pia amewahimiza watumishi kutekeleza majukumu yao kwa weledi, kuzingatia maadili ya utumishi na kulinda usiri wa taarifa za wagonjwa kwa kufuata taratibu zilizowekwa.
Mada hiyo ni sehemu ya kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa MNH linalofanyika chini ya kaulimbiu isemayo, "Pamoja tunajenga Muhimbili Imara, Bunifu na yenye huduma bora kwa kila mwananchi," likitoa fursa kwa watumishi kujifunza na kujengewa uwezo katika maeneo mbalimbali yanayochangia kuboresha utendaji na utoaji wa huduma.






No comments:
Post a Comment