Na. Mwandishi Wetu,
Mbeya
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Mhe. Solomon Itunda, amefungua rasmi Maonesho ya Biashara na Uwekezaji Nyanda za Juu Kusini (KITF 2026) yanayofanyika katika Kata ya Itezi, Jimbo la Uyole, Mkoani Mbeya.
Itunda amefungua maonesho hayo 18 Oktoba, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Mhe. Itunda amewataka wafanyabiashara kujitokeza kwa wingi kutangaza bidhaa na huduma zao na kutumia fursa ya kupanua masoko na kutumia fursa zilizopo katika sekta ya biashara na uwekezaji.
Amesema maonesho hayo yatawaunganisha wafanyabiashara, wateja na wadau mbalimbali kwa lengo la kukuza na kuchochea uchumi.
Kwa upande wake, Mratibu Msaidizi wa maonesho hayo, George Mwaitenda, amesema KITF 2026 itaonyesha bidhaa na huduma za wafanyabiashara na kuibua fursa mpya za uwekezaji.
Amesema maonesho hayo yatachangia ukuaji wa uchumi kwa kuwawezesha wadau kukutana na kubadilishana uzoefu.
Maonesho hayo mwaka huu ni msimu wa tatu yanayofanyika 16-25 Oktoba, 2026 ambapo wadau mbalimbali wakiwemo Taasisi na Mashirika ya Serikali, binafsi wanauza na kuonesha bidhaa zao.















No comments:
Post a Comment