ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, October 18, 2026

NGORONGORO YAIBUKA KIDEDEA TUZO ZA AFRIKA GHANA

 


Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imeshinda tuzo za kibiashara za Afrika zilizotolewa tarehe 17.Oktoba Mwaka huu jijini Accra nchini Ghana.

Katika tuzo hizo zilizoshirikisha mataifa,taasisi na makampuni makubwa ya kibiashara kutoka nchi za Afrika Ngorongoro iliibuka mshindi katika usimamizi wa utalii na uhifadhi endelevu.

Mgeni rasmi katika tukio hilo balozi  wa Tanzania nchini Ghana Mwenye makazi yake nchini Nigeria  mheshimiwa Selestine Kakele alizipongeza nchi za Afrika kutokana na kukua kibiashara na kuanza kukuza mitaji kutoka nchi moja hadi nyingine.

Balozi Kakele amewakaribisha wamiliki wa makampuni makubwa barani Afrika na wafanyabiashara wenye mitaji kuwekeza katika nchi ya Tanzania ambapo amesema ina usalama na upendeleo mahsusi wa kibiashhara kwa kila mwenye kutaka kufanya biashara.

Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Abdul-Razaq Badru amesema tuzo hiyo ni ishara kwamba chapa ya Ngorongoro ina hadhi ya hali ya juu kutokana na usimamizi uliotukuka wa uhifadhi na utalii.

Sherehe hiyo ilihudhuriwa na baadhi ya mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao katika nchi ya Ghana.




No comments: