Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepokea tuzo ya heshima kwa kutambuliwa kuwa hospitali ya kwanza nchini Tanzania kuanzisha huduma za tiba za dharura (Emergency Medicine Services). Tuzo hiyo imetolewa leo, Novemba 12, 2026, na Chama cha Wataalamu wa Tiba za Dharura Tanzania (EMAT), katika Kongamano la 8 la Afrika la Tiba za Dharura (AfCEM 2026), linalofanyika katika ukumbi wa Arusha International Conference Centre (AICC), jijini Arusha.
Utambuzi huo unaonesha mchango wa Muhimbili katika kuendeleza huduma za tiba za dharura nchini na juhudi zake za kuimarisha utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi ambapo katika Kongamano hilo la siku tatu, linalofanyika kuanzia Novemba 11 hadi 13, 2026, wataalamu wa tiba za dharura, madaktari na wauguzi kutoka Muhimbili wanakutana na wenzao kutoka mataifa mbalimbali hapa Afrika na maeneo mengine duniani kwa ajili ya kujadili na kubadilishana uzoefu kuhusu uimarishaji wa huduma za dharura.





No comments:
Post a Comment