ANGALIA LIVE NEWS

Friday, February 26, 2010

24 wafa Timbuktu


A picture taken on April 10, 2006 shows the Djinguereber mosque of Timbuktu, where a stampede left at least 24 people crushed to death and many more injured, officials and witnesses said on February 26, 2010.
picha ya msikiti ulioanguka Djinguereber Timbuktu na kuuwa watu wanaokadiriwa 24,picha hii ilipigwa april 10 2006

 Takriban watu 24, wengi wakiwa wanawake na watoto, wamefariki dunia kutokana na msongamano katika msikiti maarufu wa Djinguereber huko Timbuktu.
Mtafaruku huo ulitokea katika sherehe za Maulid kuadhimisha kuzaliwa kwa mtume Muhammad, wakati watu walipouzunguka msikiti huo uliotengenezwa kwa tope kaskazini mwa Mali.
Waumini walitumia njia tofauti na walioizoea kutokana na kufanyiwa ukarabati wa jengo hilo lililojengwa tangu karne ya 14.
Timbuktu, iliyopo katika jangwa la Sahara, zamani ilikuwa kituo cha mafunzo ya kiislamu.
Ripoti moja inasema tukio hilo limetokea wakati mama mmoja mtu mzima alipoanguka huku maelfu wengine wakijaribu kuzunguka msikiti huo mara tatu.

No comments: