ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, February 24, 2010

Boss wa Toyota,Akio Toyoda akalia kiti moto Congress,aomba msamaha,ahaidi kufanya kweli

Rais wa kampuni kubwa ya kutengezeza magari ya Japan, Toyota ameomba msamaha mbele ya baraza la Congress la Marekani kufuatia vifo vilivyosababishwa na kasoro kwenye magari yake.
Dosari hizo zililazimu Toyota kulazimika kurejesha mamilioni ya magari yake.
Bwana Akio Toyoda alikabiliwa na wakati mgumu kujibu maswali kutoka kwa wabunge wa Congress waliokuwa na ghadhabu. Wabunge hao waliishutumu kampuni ya Toyota ambayo walisema inachochewa na ulafi na kutojali maslahi ya wateja.
Toyota imelaumiwa kwa kulegea katika kutatua kasoro ya breki za magari yake.

No comments: