ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, February 24, 2010

Ishu ya manyoya ya paka inatulostisha!

Baada ya lile sakata la uvumi ulionea jijini dsm wiki iliyopita kuhusu mwanamke aliyebadilishwa mkono wake kuwa na manyoya ya paka kabla ya kutoweka kimaajabu baada ya kumsaidia ombaomba.

Watu wenye ulemavu wamekuja juu kwa kuvilaumu vyombo vya habari kwa kile walichokiita jamii kuwanyanyapaa, kutokana na habari za uvumi huo zilizoenezwa kupitia vyombo mbalimbali vya minews.

Walemavu hao ambao walikutana na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa habari na maelezo...walitoa dukuduku lao, wakilalamikia vyombo vya habari kwa kile walichodai kueneza uvumi ambao umewaweka pabaya.

Wakifafanua zaidi malalamiko yao walidai kuwa wamekuwa wakinyanyasika kwa jamii wakiwamo wenye nyumba wanazopanga, kwa kuwataka kuhama na hata kukejeliwa na watu ndani ya mabasi wakiwataka kutowagusa kwa hofu ya kugeuzwa kuwa na manyoya ya paka.

No comments: