Mlinzi wa Manchester City Wayne Bridge amejiondoa katika kikosi cha timu ya taifa ya England na hatoichezea timu hiyo katika mashindano ya Kombe la Dunia.Katika taarifa iliyotolewa na mawakili wake, Bridge mwenye umri wa miaka 29, amesema nafasi yake katika kikosi cha timu ya taifa ameona haitakuwa na "ufanisi na anaepusha mgawanyiko".
Mlinzi huyo wa upande wa kushoto amekuwa akitajwa kuhusiana na tuhuma za mpenzi wake wa zamani kuwa na uhusiano na John Terry.
Kocha wa England Fabio Capello mwezi huu alimvua unahodha Terry.
Katika taarifa hiyo ya Bridge iliyotolewa siku ya Alhamisi, ameongeza kusema amefikiria kwa muda mrefu nafasi yake katika kikosi cha England na hasa akihusisha matukio yaliyokuwa yakiarifiwa kwa wiki kadha.
Ameendelea kusema ni jambo la heshima kila wakati kuichezea England. Hata hivyo baada ya kufikiria kwa makini anaamini nafasi yake katika kikosi hicho kwa sasa haitakuwa na ufanisi na huenda kungesababisha mgawanyiko.
No comments:
Post a Comment